KAULI YA CHINA KWA UKRAINE NA URUSI
China imesema inafuatilia kwa ukaribu mzozo kati ya Urusi na Ukraine na kuilaumu Marekani kuwa inachochea mzozo huo ili iendelee kuuza silaha za kivita kwa Ukraine "Tunaziomba pande zote mbili kufungua milango ya mazungumzo ya amani badala ya kuendeleza vurugu"
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China, Hua Chunying, amesema "Marekani inachochea vita na mzozo wa Urusi na Ukraine kwa muda mrefu sasa huku ikinufaika na mzozo huo kwa kuiuzia Ukraine silaha zenye thamani ya zaidi ya USD Bilioni 1.5, sio sawa kuwanyooshea vidole Watu kwa moto uliouchochea mwenyewe"
"Baadhi ya Vyombo vya Habari vinatumia neno 'Uvamizi' kwamba Urusi imeivamia Ukraine lakini Vyombo hivi vilitumia neno gani wakati Marekani ilipofanya uvamizi kama huo na vitendo vya kivita dhidi ya Afghanistan na Iran bila kibali cha kisheria kutoka Umoja wa Mataifa!?"
Kauli hiyo ya China dhidi ya mataifa hayo ni ya kutaka amani.
Comments