Posts

Showing posts with the label Habari za Kitaifa

MCHENGERWA: MIRADI YOTE NGAZI YA MSINGI ITANGAZWE KUPITIA NeST

Image
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na wakuu wa vitengo vya manunuzi kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa katika ngazi ya msingi inatangazwa kupitia mfumo wa NeST. Akizungumza leo jijini Dodoma katika kikao kazi na wabunge, wakurugenzi wa halmashauri, makatibu tawala wasaidizi miundombinu na wakuu wa vitengo vya manunuzi, Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa utekelezaji wa miradi lazima ufuate sheria za manunuzi na kuanzia sasa utatangazwa kupitia NeST pekee. Ameeleza kuwa baada ya mafunzo haya, wahusika wanapaswa kubadilika na kusimamia miradi kwa weledi na uaminifu ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana. Pia, ameitaka PPRA kuwajengea uwezo watumiaji wa NeST katika ngazi za msingi ili kupunguza changamoto wakati wa mchakato wa zabuni.

TANZANIA YATEULIWA NA SOMALIA KUSHIRIKIANA KATIKA UGAVI WA BIDHAA ZA AFYA

Image
Wizara ya Afya nchini Somalia imeichagua Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kushirikiana kwenye masuala mbalimbali yanayohusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa kubadilishana uzoefu katika maeneo ya mifumo, ununuzi, usambazaji na udhibiti ubora. Hayo yamebainishwa na watendaji wa Wizara ya Afya kutoka Somalia waliotembelea Bohari ya Dawa (MSD), ambapo mwakilishi wa ugeni huo, Mohamed Abdulukadiri Hersi, ameeleza kuwa hatua mbalimbali zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia MSD katika mifumo ya ugavi inayotumia teknolojia ndio zimewavutia zaidi kuja kujifunza kwa kujionea namna inavyofanya kazi na kulinganisha na mifumo mingine ya serikali. Hersi ameongeza kuwa Somalia ipo kwenye mpango wa kujenga upya mfumo wake wa ugavi wa bidhaa za afya, ikiwa ni pamoja na kuboresha utaratibu wa kufikisha bidhaa za afya kwa wananchi. Amesema kati ya nchi walizozichagua kuwa mfano ni Tanzania, ambapo kupitia MSD wamejifunza mengi ambayo watakwenda kuyatekeleza watakaporudi. Naye Mkurugenz...

RAIS DKT. SAMIA KUANDIKA HISTORIA KWA KUPATA TUZO YA KIMATAIFA KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA AFYA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kupokea tuzo ya kimataifa ya The Gates Goalkeepers Award, ikiwa ni ishara ya kutambua mafanikio makubwa aliyoyapata katika uongozi wake, hususan katika kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi. Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa Demografia na Afya ya mwaka 2022, Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya uzazi kwa asilimia 80, mafanikio yanayoifanya kuwa moja ya nchi zinazopiga hatua kubwa katika kuboresha afya ya mama na mtoto. Akizungumza jijini Dar es Salaam Februari 3, 2025, Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, alisema kuwa tukio hilo la utoaji wa tuzo linaloratibiwa na Taasisi ya The Gates Foundation litafanyika kwa mara ya kwanza nje ya Marekani, na Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji. Rais Samia Suluhu Hassan anakuwa kiongozi wa kwanza barani Afrika kupokea tuzo hiyo, hatua inayodhihirisha kutambuliwa kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya sekta ya afya na ustawi wa jamii. “Hii ni h...

SERIKALI YAZIDI KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA AKILI KWA KULETA MAPINDUZI KATIKA MAFUNZO NA AJIRA ZA WATAALAM

Image
Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa wataalam wa afya ya akili nchini kwa kuwajengea uwezo wataalam 2,980 kutoka vituo 710 vya afya kote nchini ili waweze kutoa huduma hizo kwa ufanisi katika maeneo yao. Hatua hii inalenga si tu kuongeza idadi ya wataalam waliobobea katika afya ya akili, bali pia kuhakikisha kuwa huduma hizo zinapatikana kwa urahisi katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya, hususan kwa wananchi walioko vijijini. Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Jesca Jonathani Msambatavangu, Bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema kuwa Serikali inaendelea kupanua sekta ya afya ya akili kwa kuajiri wataalam zaidi na kuimarisha mafunzo kwa madaktari na wahudumu wa afya. “Kwa mwaka 2024 pekee, Serikali imeajiri jumla ya watumishi wapya 56 katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, ikiwa ni jitihada za kupunguza uhaba wa wataalam wa sekta hii muhimu,” alisema Dkt. Mollel. Katika...

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA

Image
Rais wa Jamhuri ya Cabo Verde, Mhe. José Maria Pereira Neves, amezihimiza nchi za Afrika kuimarisha demokrasia na utawala bora ili kuepuka kurudia makosa ya kihistoria yaliyoletwa na ukoloni, ambayo hadi sasa yameziacha baadhi ya nchi zikiendelea kudai fidia. Mhe. Neves alitoa kauli hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mwaka Mpya wa Mahakama ya Umoja wa Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, hafla iliyofanyika jijini Arusha. Alionya kuwa migogoro inayoendelea kushuhudiwa barani Afrika inaathiri maendeleo ya kijamii, huku sababu kuu ikiwa ni ukosefu wa haki za binadamu na uongozi bora. “Naipongeza Mahakama ya Umoja wa Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kwa kuchagua kaulimbiu inayosisitiza ulipaji wa fidia kama njia ya kuendeleza haki kwa watu wa Afrika. Hata hivyo, fidia ni zaidi ya malipo ya kifedha—ni mchakato wa uponyaji wa majeraha ya kihistoria. Hatutakiwi kuishia kulaani na kukemea tu, bali tunapaswa kuchukua hatua za kweli. Vinginevyo, vizazi vijavyo vitadai fidia si kwa wa...

RAIS SAMIA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA TANZANIA

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Chinangali, Jijini Dodoma, mnamo tarehe 3 Februari 2025. Hafla hiyo muhimu, ambayo huadhimishwa kila mwaka, ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, majaji, mawakili, maofisa wa serikali, na wadau wengine wa sekta ya sheria. Katika hotuba yake, Rais Samia alisisitiza umuhimu wa mfumo wa sheria imara katika maendeleo ya taifa, akibainisha kuwa utawala wa sheria ni msingi wa haki, amani, na maendeleo endelevu. Aliwataka wadau wa sheria, wakiwemo mawakili na majaji, kuendelea kuwa mfano wa uadilifu na uwajibikaji katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati na bila upendeleo. “Tunapoadhimisha Siku ya Sheria, napenda kusisitiza kuwa uwajibikaji wa vyombo vya sheria ni muhimu katika kuleta imani ya wananchi kwa serikali na taasisi za kisheria. Hatuna budi kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa wote kwa usawa,” alisema R...

WAKANDARASI WAJENGE BARABARA ZA TACTIC KWA WAKATI – MHANDISI MATIVILA

Image
  NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila, amewataka wakandarasi wanaojenga barabara za Engosheraton, Olasiti, na Oljoro jijini Arusha kuhakikisha zinakamilika kwa wakati ili kuwezesha maendeleo ya miundombinu katika jiji hilo. Mhandisi Mativila alitoa agizo hilo wakati wa ziara yake kwenye barabara hizo, ambazo zinajengwa kupitia Mradi wa Kuboresha Miji (TACTIC) chini ya TARURA. Barabara hizo zina urefu wa kilomita 12.1 na thamani ya shilingi bilioni 15.4, lakini utekelezaji wake bado uko nje ya muda uliopangwa. “Barabara hizi zinapaswa kuwa zimefikia asilimia 99 ya ujenzi, lakini hadi sasa kazi haijakamilika. Wakandarasi lazima wahakikishe mradi huu unakamilika ifikapo Juni mwaka huu,” alisema Mhandisi Mativila. Aliongeza kuwa barabara ya Oljoro bado ipo nyuma kwa asilimia 35 kutokana na mabadiliko ya usanifu wake, kwani sasa imepandishwa hadhi kuwa barabara ya mkoa kutokana na uwepo wa stendi mpya ya mabasi inayojengw...

RAIS SAMIA AZINDUA SERA MPYA YA ELIMU, AZITAKA WIZARA HUSIKA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WAKE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa uwepo wa Sera Mpya ya Elimu na Mitaala Mipya pekee haviwezi kuleta matokeo chanya bila utekelezaji makini. Akizungumza Februari 1, 2025, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 – Toleo la 2023, Rais Samia ameagiza wizara husika kuhakikisha kuwa utekelezaji wa sera hiyo unafanyika kikamilifu ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa. “Naitaka Wizara ya Fedha, Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na TAMISEMI kuwezesha na kusimamia utekelezaji wa sera na mitaala hii mpya kwa ufanisi,” amesema Rais Samia. MAGEUZI KATIKA SEKTA YA ELIMU Katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza kuwa maboresho hayo lazima yawazingatie walimu kwa kuwapatia mafunzo sahihi, kuwaajiri wenye sifa stahiki, na kuboresha maslahi yao. Aidha, ameweka wazi kuwa dhamira ya mabadiliko haya ni kumuandaa kijana mwenye kujiamini na aliye tayari kushindana katika soko la...

SERIKALI YAELEZA GHARAMA ZA KUUNGANISHA UMEME VIJIJINI

Image
Dodoma, 30 Januari 2025 – Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa gharama ya kuunganisha umeme katika maeneo ya vijiji ni Shilingi 27,000, huku maeneo ya vijiji mji gharama ikiwa Shilingi 360,960. Mhe. Kapinga alitoa ufafanuzi huo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Bukene, Mhe. Selemani Zedi, aliyependa kufahamu kwa nini maeneo ya Bukene na Itobo hayaunganishiwi umeme kwa gharama ya Shilingi 27,000. “Mheshimiwa Spika, maeneo ya Bukene na Itobo ni vijiji mji, hivyo yanafuata gharama ya Shilingi 360,960,” alisisitiza Mhe. Kapinga. Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kufanya tathmini ili kuona uwezekano wa kufanya maboresho ya gharama hizo. Aidha, tayari amemuagiza Meneja wa Mkoa wa Tabora na wa Wilaya ya Nzega kufanya tathmini ya kina ili kuondoa mkanganyiko uliopo kuhusu gharama za uunganishaji wa umeme katika maeneo hayo. Katika hatua nyingine, akijibu swali la Mbunge wa K...

MOI KUANZA USAJILI WA WAGONJWA KWA KUTUMIA NAMBA YA NIDA KUANZIA FEBRUARI 1

Image
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imetangaza kuwa kuanzia tarehe 1 Februari 2025, usajili wa wagonjwa utaanza kufanyika kwa kutumia namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA). Hatua hii inalenga kuboresha mfumo wa utambuzi wa wagonjwa, kuhakikisha upatikanaji wa taarifa zao kamili, na kuweka kumbukumbu sahihi kwa uboreshaji wa huduma za afya. Pia, itarahisisha usomaji na ubadilishanaji wa taarifa za mgonjwa kati ya taasisi mbalimbali za matibabu, kupunguza mkanganyiko wa taarifa, na kusaidia ndugu kumtambua mgonjwa endapo atashindwa kujitambulisha. Menejimenti ya MOI imewataka wagonjwa wote wanaofika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu kuhakikisha wanakuwa na Kitambulisho cha Taifa. Kwa wale ambao bado hawajapata kitambulisho hicho, watalazimika kuwasilisha barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa, Sheha, au Kijiji wanachoishi. Uwasilishaji wa barua hizo utafanyika hadi tarehe 30 Juni 2025. MOI inawahimiza wananchi kuchukua hatua mapema ili kuepusha usumbufu wakati...

ZAIDI YA ASILIMIA 97 YA WATU WAPATIWA DAWA ZA KINGATIBA YA MATENDE NA MABUSHA NCHINI

Image
 Serikali kupitia Wizara ya Afya imefanikiwa kuwapatia dawa za kingatiba ya matende na mabusha kwa wananchi 257,358 kati ya walengwa 265,217, sawa na asilimia 97, katika Halmashauri za Mtama na Mtwara Mikindani kwa mwaka 2024. Hatua hii ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kudhibiti na kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini. Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, ametoa takwimu hizo Januari 30, 2025, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Duniani. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Tuungane, Tuchukue Hatua, Tutokomeze Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele.” Kwa upande wa ugonjwa wa usubi, watu milioni 5,462,851 kati ya milioni 6,447,157 kutoka halmashauri 24 walipatiwa kingatiba, ikiwa ni sawa na asilimia 85 kwa mwaka 2024. Aidha, kuhusu ugonjwa wa trakoma, Waziri Mhagama amebainisha kuwa watu milioni 1,603,425 kati ya milioni 1,967,143 kutoka hadi halmashauri saba (Ngorongoro, ...

WAZIRI BASHE AONGOZA KIKAO NA BODI YA PAMBA KUJADILI MUSTAKABALI WA TASNIA

Image
Tarehe 30 Januari 2025, Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb), aliongoza kikao kazi na Wajumbe wa Bodi ya Pamba jijini Dodoma. Lengo kuu la kikao hicho lilikuwa kujadili masuala mbalimbali yanayohusu tasnia ya pamba nchini, ikiwa ni pamoja na mikakati ya kuongeza uzalishaji, kuboresha ubora wa pamba, na kuhakikisha masoko ya uhakika kwa wakulima. Katika kikao hicho, Waziri Bashe alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, wakulima, na wadau wengine katika mnyororo wa thamani wa pamba ili kufikia malengo ya kuongeza tija na kipato kwa wakulima. Pia, alihimiza matumizi ya mbegu bora, mbolea, na teknolojia za kisasa katika kilimo cha pamba ili kuongeza uzalishaji na ubora wa zao hilo. Aidha, Waziri Bashe aliitaka Bodi ya Pamba kuhakikisha inasimamia vyema masoko ya pamba na kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri na ya haki kwa mazao yao. Alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima na wawekezaji katika sekta ya pamba ili kuhakikisha tasnia hiyo ...

RAIS DKT. SAMIA KUSHIRIKI MKUTANO WA DHARURA WA SADC NCHINI ZIMBABWE KUJADILI HALI YA ULINZINA USALAMA DRC

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kusafiri leo Januari 31, 2025, kuelekea Harare, Zimbabwe kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Akiwa nchini Zimbabwe, Rais Dkt. Samia atashiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC ulioitishwa kujadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mkutano huo utaongozwa na Rais wa Zimbabwe na Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Dkt. Emmerson Dambudzo Mnangagwa. Mkutano huu unafanyika kufuatia Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ Troika) pamoja na nchi zinazochangia askari katika Misheni ya SADC nchini DRC (SAMIDRC), uliofanyika Januari 28, 2025, chini ya uenyekiti wa Rais Dkt. Samia.NA USALAMA DRC Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya...

BIASHARA KARIAKOO KUFANYIKA SAA 24 UZINDUZI FEBRUARI 22,2025

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametangaza kuwa biashara katika Soko la Kariakoo zitaanza kufanyika saa 24. Uzinduzi rasmi wa mfumo huo utafanyika Februari 22, ukianzia katika ofisi za Mkuu wa Mkoa hadi Kariakoo. RC Chalamila amesema hatua hii inalenga kuongeza fursa za kiuchumi, kuboresha mazingira ya biashara, na kuhakikisha wafanyabiashara wanapata muda wa kutosha kuhudumia wateja wao bila vikwazo vya muda. Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa biashara na usalama imejipanga kuhakikisha mazingira yanakuwa salama kwa wafanyabiashara na wateja katika kipindi chote cha biashara saa 24. Taarifa zaidi kuhusu utaratibu wa utekelezaji wa mfumo huu zitaendelea kutolewa kwa umma.

WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUANZA KUREJESHWA SOKONI FEBRUARI 2025

Image
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Masoko Kariakoo, Mhe. Hawa Ghasia, amesema kuwa kazi ya kuwarejesha wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo itaanza mapema Februari 2025. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika ukumbi mdogo wa TAMISEMI, Bi. Ghasia alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa soko hilo pamoja na uhakiki wa waliokuwa wafanyabiashara wake. Uhakiki huo ulifanywa na Timu Maalum iliyoundwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na wawakilishi wa wafanyabiashara, Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo, na vyombo vya usalama. “Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika, ninapenda kuwajulisha wananchi na wafanyabiashara kuwa Soko la Kariakoo litaanza rasmi kurejesha shughuli zake kuanzia Februari 2025,” alisema Bi. Ghasia. Aliongeza kuwa Menejimenti ya shirika hilo inaendelea kuratibu kazi ya kutangaza majina ya waliokuwa wafanyabiashara wa soko hilo ambao wamekidhi vigezo na sifa...

SERIKALI YAJIPANGA KIKAMILIFU KUKABILIANA NA MARBURG

Image
  Serikali inaendelea na juhudi za kudhibiti ugonjwa wa Marburg tangu ulipotangazwa kwa mara ya kwanza Januari 19, 2025, wilayani Biharamulo, mkoani Kagera. Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Dkt. Ntuli Kapologwe, alieleza Januari 24, 2025, kuwa wizara imeweka kambi wilayani humo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wahisiwa wa ugonjwa huo, sambamba na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujikinga na kutambua dalili za ugonjwa huo. Mpaka sasa, idadi ya waliofariki ni wawili, wagonjwa wahisiwa ni 15, huku watu 281 waliokuwa karibu na waathirika wakiendelea kufuatiliwa. “Serikali imeimarisha udhibiti wa ugonjwa huu kwa kuleta madaktari bingwa, vifaa vya upimaji, madawa, pamoja na kuwashirikisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii, ambao wanapita nyumba kwa nyumba kubaini wahisiwa wa ugonjwa huo,” alisema Dkt. Kapologwe. Kwa mujibu wa Dkt. Kapologwe, wahudumu wa afya ngazi ya jamii 191 walioko kwenye mafunzo kwa vitendo wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za awali za matibabu kwa wananc...

BUNGE LAPITISHA MAREKEBISHO YA SHERIA 12 KUBORESHA UTEKELEZAJI

Image
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Miswada Miwili ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya 2024 Januari 29, 2025, katika kikao cha pili cha Mkutano wa 18 wa Bunge hilo. Miswada hiyo ni: 1. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mbalimbali (Na.3) wa Mwaka 2024 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments No. 3) Bill 2024) 2. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2024 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments No. 4) Bill 2024) Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari, amesema Miswada hiyo inalenga kufanya marekebisho kwenye jumla ya sheria 12 ili kuboresha utekelezaji wake na kuzifanya ziendane na mahitaji ya sasa kwa manufaa ya wananchi. Miongoni mwa sheria zilizofanyiwa marekebisho ni Sheria ya Mawakili, Sheria ya Madini, Sheria ya Utumishi wa Umma, Sheria ya Kudhibiti Utakatishaji wa Fedha Haramu, Sheria ya Vyama vya Ushirika, na Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawa...

WATANZANIA WALIOKWAMA VITANI DRC WAOKOLEWA

Image
Mapigano yaendelea kushika kasi, waasi wa M23 waendelea kusonga mbele Raia wa Tanzania waliokuwa wamekwama katika machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hatimaye wameokolewa baada ya kuomba msaada kufuatia mapigano makali. Watanzania hao walijikuta katikati ya vita baada ya waasi wa M23 kushambulia na kuteka maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na Goma. Wengi walilazimika kujificha katika eneo la Jambo Safari na Uwanja wa Ndege wa Goma, huku milio ya risasi na makombora ikiendelea kusikika karibu nao. Mashirika ya misaada na vikosi vya usalama vya Kongo vilihusika katika juhudi za kuwaokoa raia hao, ambao walikuwa hatarini kutokana na hali mbaya ya usalama. Mapigano kati ya waasi wa M23 na majeshi ya Kongo (FARDC) yanaendelea kushuhudiwa mashariki mwa DRC, huku hali ikiendelea kuwa mbaya zaidi, ikiwalazimu maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao.

MARAIS WA AFRIKA WAAZIMIA KUWAUNGANISHA WAAFRIKA MILIONI 300 KWENYE NISHATI

Image
Trilioni 110/- zatengwa kwa ajili ya mpango wa MISSION300 Marais wa Afrika wameazimia kuchukua hatua kubwa katika kuhakikisha upatikanaji wa nishati barani Afrika, wakitenga jumla ya trilioni 110/- ili kuwaunganisha Waafrika milioni 300 kwenye huduma za nishati. Mpango huo, unaojulikana kama MISSION300, unalenga kuboresha maisha ya mamilioni ya watu ambao bado hawajafikiwa na nishati ya uhakika, huku viongozi wakisisitiza umuhimu wa usimamizi bora wa fedha hizi ili kuhakikisha matokeo chanya kwa wananchi. “Tunataka kuona matokeo chanya kwa hawa watu milioni 300 watakaoguswa na MISSION300, lakini tunasisitiza umuhimu wa kusimamia fedha vizuri,” alisema mmoja wa viongozi katika mkutano huo. Mpango huu unatarajiwa kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya nishati, kupunguza umaskini wa nishati, na kuongeza fursa za kiuchumi kwa jamii mbalimbali barani Afrika.

UFUNGUZI WA MKUTANO WA VIONGOZI WA AFRIKA KUHUSU NISHATI JIJINI DAR ES SALAAM: MISHENI 300

Image
  • Dkt. Doto Biteko: Tanzania imeongeza uwezo wa kuzalisha umeme kutoka megawati 21 mwaka 1960 hadi megawati 3,160 sasa, na inalenga kufikia megawati 4,000 ifikapo 2025. • Ajenda ya Mkutano: Kupanua upatikanaji wa umeme kwa Waafrika milioni 300 ndani ya miaka mitano, kupunguza hewa ukaa, na kuboresha maisha ya watu. • Wadau: Benki ya Dunia, AfDB, SEforALL, GEAPP, na wengine wamesaidia kufanikisha mkutano huu. • Mafanikio ya Tanzania: Umeme umefikishwa vijijini vyote 12,318, huku miundombinu ikihusisha Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi. • Rais Samia: Amejikita kukuza suluhisho la nishati safi ya kupikia Afrika. MAAZIMIO NA MALENGO YA MKUTANO • Kupanua nishati mbadala. • Kufungua uwekezaji wa sekta binafsi. • Kuanzisha Kiashiria cha Ufuatiliaji wa Maazimio. MATAMSHI YA VIONGOZI WENGINE • Ajay Banga (WB): “Tunaweza kubadilisha sura ya Afrika kwa juhudi za pamoja.” • Dkt. Akinumwi Adesina (AfDB): “Tanzania ni mfano wa kuigwa katika uwekezaji wa ...