Posts

Showing posts with the label Teuzi

DKT. SAMIA AMTEUA DKT. MPOKI KUWA BOSI MPYA MOI

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali leo nchini. Aidha, amemteua Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI). Pia amemteua Bi. Joyce Gideon Mapunjo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Bi. Mapunjo anachukua nafasi ya Mhandisi Musa Iyombe ambaye amemaliza muda wake. Taarifa za uteuzi huo zimetolewa leo 02 Disemba 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga.

MHANDISI PETER ULANGA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI ATCL

Image
  Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Novemba 2024 amefanya teuzi ifuatavyo. Amemteua Mhandisi Peter Rudolf Ulanga  kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) akichukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amestaafu. Rais Samia pia amemteua Prof. Harun Jeremia Mapesa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kabla ya uteuzi huu, Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe na anachukua nafasi ya Prof. Shadrack Mwakalila ambaye amemaliza muda wake.