MHANDISI PETER ULANGA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI ATCL
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Novemba 2024 amefanya teuzi ifuatavyo.
Amemteua Mhandisi Peter Rudolf Ulanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) akichukua nafasi ya Mhandisi Ladislaus Matindi ambaye amestaafu.
Rais Samia pia amemteua Prof. Harun Jeremia Mapesa kuwa Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, kabla ya uteuzi huu, Prof. Mapesa alikuwa Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Mzumbe na anachukua nafasi ya Prof. Shadrack Mwakalila ambaye amemaliza muda wake.

Comments