WATOTO WA MAREHEMU MEJA JENERALI MBUGE WADAI HAKI ZAO KWA TRA NA BRELA
Watoto watatu wa Marehemu Meja Jenerali Charles Mang’era Mbuge (Mstaafu) wameandika barua rasmi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakidai haki yao ya kisheria baada ya kifo cha baba yao. Watoto hao, Imani Charles Mbuge, Elizabeth Charles Mbuge, na Marietha Charles Mbuge, wanataka mamlaka hizo kufunga “TIN” namba na leseni za marehemu baba yao kwenye mali zilizopo Kitunda Relini, Dar es Salaam, na Kisarawe, Pwani. Kwa mujibu wa barua yao, mali zinazohusika ni Jakicha Motel , iliyopo Kitunda Relini, Dar es Salaam, na shamba la biashara lililopo Kisarawe, Pwani. Wamedai kuwa tangu kifo cha baba yao, kilichotokea tarehe 12 Oktoba 2024 katika Hospitali ya Apollo nchini India, hawajapokea mgao wowote wa fedha licha ya marehemu kuwa na umiliki wa asilimia 80 ya hisa katika Jakicha Motel. Watoto hao wametoa muda wa siku mbili, hadi kufikia tarehe 1 Januari 2025, kwa mamlaka zinazohusika kuhakikisha wanapokea kiasi cha shilingi m...