Posts

Showing posts with the label Uteuzi

DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI WA MAKAMISHNA WA JESHI LA POLISI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Disemba 9,2024 amefanya mabadiliko makubwa katika Jeshi la Polisi kwa kuteua makamishna wapya.  • DCP Kombo Khamis Kombo amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar, akichukua nafasi ya CP Hamad Khamis Hamad, ambaye sasa ni Balozi.  • DCP Tatu Rashid Jumbe ameteuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, akichukua nafasi ya CP Suzan Kaganda, ambaye pia ameteuliwa kuwa Balozi.

RAIS DKT. SAMIA AIHAMISHA SEKTA YA HABARI KUTOKA WIZARA YA MAWASILIANO KWENDA WIZARA YA UTAMADUNI NA MICHEZO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Disemba 8, 2024 ametangaza mabadiliko ya kiutendaji kwa kuihamisha Sekta ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Aidha  Dkt. Samia sambamba na hilo amefanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt.Moses Kusiluka, uteuzi na mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo: MAWAZIRI WALIOTEULIWA  2. Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.): Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.  3. Mhe. Jerry William Silaa (Mb.): Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.  4. Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.): Waziri wa Katiba na Sheria.  5. Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (Mb.): Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).  6. Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.): Waziri wa Mifugo na Uvuvi.  7. Mhe. Abdall...

DKT SAMIA AMKUMBUKA IGP MSTAAFU SAID MWEMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania- (IGP) mstaafu, Said Ally Mwema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania (TSN).  Aidha IGP mstaafu Mwema anachukua nafasi ya Hab Mkwizu aliyemaliza muda wake. Taarifa za uteuzi huo zimetolewa leo Novemba 27, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga.