DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI WA MAKAMISHNA WA JESHI LA POLISI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Disemba 9,2024 amefanya mabadiliko makubwa katika Jeshi la Polisi kwa kuteua makamishna wapya.
• DCP Kombo Khamis Kombo amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar, akichukua nafasi ya CP Hamad Khamis Hamad, ambaye sasa ni Balozi.
• DCP Tatu Rashid Jumbe ameteuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, akichukua nafasi ya CP Suzan Kaganda, ambaye pia ameteuliwa kuwa Balozi.

Comments