Posts

Showing posts with the label Tanzia

AJALI ILIYOUA 6 MBINGA: MIILI YA WALIOFARIKI YAAGWA RC RUVUMA AONGOZA WAOMBOLEZAJI

Image
  Disemba 28 mwaka jana, ajali ya kusikitisha ilitokea katika eneo la Chunya, wilayani Mbinga, ambapo watu sita walipoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria kushika moto.  Miili ya marehemu hao (Mabaki ya miili) wakiwemo walimu wanne, mfamasia mmoja, na dereva wa gari, imeagwa rasmi Januari 3 katika uwanja wa michezo wa Mbinga. SHUGHULI YA KUAGA Hafla hiyo imehudhuriwa na mamia ya waombolezaji waliokusanyika kuonyesha heshima zao za mwisho. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas, ameongoza mazishi hayo akitoa pole kwa familia za marehemu na kuwataka wananchi kuwa waangalifu zaidi wanapokuwa barabarani. MAREHEMU WALIOFARIKI • Walimu wanne walikuwa wakielekea wilaya ya Nyasa kwa usaili wa matumizi ya mfumo wa BVR. • Mfamasia mmoja ambaye ni mtumishi wa afya. • Dereva wa gari, aliyekuwa akiendesha gari hilo wakati wa ajali. CHANZO CHA AJALI Kwa mujibu wa taarifa za awali, ajali hiyo ilisababishwa na gari hilo kupata hitilafu kabla ya kushika moto, na juh...

WALIMU WANNE WA SHULE MOJA WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI

Image
Watu sita wakiwemo walimu wanne wa shule moja  wamefariki dunia  Katika ajali ya gari iliyotokea leo, Disemba 28, 2024, katika eneo la Chunya, mpakani mwa wilaya za Mbinga na Nyasa.  Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Prado lenye namba za usajili T 647 CVR, ambalo lilikuwa likisafiri kutoka shule ya msingi Lumaru kwenda shule ya sekondari Limbo kwa ajili ya mafunzo ya utumiaji wa BVR. Kwa mujibu wa Katibu Tawala Wilaya ya Nyasa, Salumu Mohamedi, ajali ilitokea majira ya saa mbili asubuhi, ambapo gari hilo liliteleza katika mteremko mkali wa Chunya wilayani Mbinga, kisha kuanguka na kuwaka moto. Katika ajali hiyo, walimu hao wanne kutoka shule ya msingi Lumaru, mfamasia mmoja, na dereva wa gari hilo walipoteza maisha. Maafisa wa usalama wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali na kutoa msaada kwa familia zilizopatwa na msiba huu mkubwa. Tunatoa pole kwa familia, wanafunzi, na jamii kwa jumla kwa msiba huu mkubwa.

MKUU WA MAJESHI ATANGAZA KIFO CHA MEJA JENERALI MARTIN BUSUNGU (MSTAAFU)

Image
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, ametangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Meja Jenerali Martin Shiminzi Busungu (Mstaafu) ambaye  amefariki dunia tarehe 24 Desemba 2024, majira ya saa 10:15 jioni, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Enzi za utumishi wake, Meja Jenerali Busungu alishikilia nyadhifa mbalimbali muhimu, zikiwemo: • Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT): Aliongoza kuanzia mwaka 2018 hadi 2019. • Mkuu wa Jeshi la Akiba (Mgambo): Alihudumu kuanzia mwaka 2019 baada ya kuhama kutoka JKT. Wakati wa uongozi wake, alisimamia miradi mingi ya maendeleo, ikiwemo uzinduzi wa Kiwanda cha Kuchakata Mahindi cha Mlale JKT huko Songea, mkoani Ruvuma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, ratiba ya utoaji wa heshima za mwisho na mazishi ya marehemu itatangazwa baadaye. Mungu ailaze roho ya Meja Jenerali Busung...

RATIBA YA MAZISHI WA MHE. DKT. NDUGULILE

Image
 

FAUSTINE NDUNGULILE AMEFARIKI DUNIA

Image
Mbunge wa Kigamboni DK Faustine Ndugulile amefariki dunia tarehe 27 Novemba 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu. Taarifa ya kifo hicho imetolewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson. Amesema taarifa zaidi kuhusu msiba huo itatolewa. Dk Ndugulile Alikuwa Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Dunia Kanda ya Afrika (WHO) ambaye alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari 2024. "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu allaze roho ya marehemu mahali pema peponi,"amesema Spika