WALIMU WANNE WA SHULE MOJA WAFARIKI KATIKA AJALI YA GARI


Watu sita wakiwemo walimu wanne wa shule moja  wamefariki dunia  Katika ajali ya gari iliyotokea leo, Disemba 28, 2024, katika eneo la Chunya, mpakani mwa wilaya za Mbinga na Nyasa. 

Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Prado lenye namba za usajili T 647 CVR, ambalo lilikuwa likisafiri kutoka shule ya msingi Lumaru kwenda shule ya sekondari Limbo kwa ajili ya mafunzo ya utumiaji wa BVR.


Kwa mujibu wa Katibu Tawala Wilaya ya Nyasa, Salumu Mohamedi, ajali ilitokea majira ya saa mbili asubuhi, ambapo gari hilo liliteleza katika mteremko mkali wa Chunya wilayani Mbinga, kisha kuanguka na kuwaka moto.


Katika ajali hiyo, walimu hao wanne kutoka shule ya msingi Lumaru, mfamasia mmoja, na dereva wa gari hilo walipoteza maisha.


Maafisa wa usalama wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali na kutoa msaada kwa familia zilizopatwa na msiba huu mkubwa.


Tunatoa pole kwa familia, wanafunzi, na jamii kwa jumla kwa msiba huu mkubwa.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA