Posts

Showing posts with the label Dini

VIONGOZI WAPYA WA SYRIA WATANGAZA KRISMASI KUWA SIKUKUU YA TAIFA

Image
Syria imechukua hatua ya kihistoria baada ya viongozi wapya wa serikali kutangaza rasmi kwamba Krismasi, tarehe 25 na 26 Desemba, itakuwa sikukuu ya taifa. Uamuzi huu wa Disemba 24,2024 unalenga kuheshimu na kutambua mchango wa jamii ya Wakristo nchini humo, huku taifa likijaribu kuonyesha mwelekeo wa ujumuishi baada ya kuangushwa kwa utawala wa Rais Bashar al-Assad. Hata hivyo, hali ya wasiwasi bado ipo, hasa baada ya matukio ya uchomaji wa mti wa Krismasi katika mji wa Kikristo wa Al-Suqaylabiyah, hali iliyosababisha maandamano ya Wakristo wakitaka usalama zaidi kwa maeneo yao ya ibada na urithi wa kidini. Licha ya ahadi za uongozi mpya, ambao unajumuisha wanachama wa kundi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS), jamii ya Wakristo inabaki na mashaka kutokana na historia ya kundi hilo. Wito wa kuhifadhi haki na usalama wa wachache unazidi kushika kasi wakati taifa hilo likianza safari mpya ya kisiasa. Hatua hii inatafsiriwa kama ishara ya matumaini, lakini Wakristo wa Syria wanataka vitendo za...

POLISI WAMKAMATA MWANAUME ALIYESEMA “MIMI NI MKRISTO” UJERUMANI

Image
Katika tukio lililozua mjadala mkali nchini Ujerumani, polisi wamemkamata mwanaume aliyekuwa akisema, “Mimi ni Mkristo,” katika mji wa Magdeburg. Kisa hicho kilitokea mnamo Desemba 21, 2024, muda mfupi baada ya tukio la kusikitisha ambapo gari liliingia katika umati wa watu kwenye soko la Krismasi, na kusababisha vifo kadhaa pamoja na majeruhi. Kwa mujibu wa ripoti, video ya tukio hilo inaonyesha polisi wakimziba mdomo mwanaume huyo kabla ya kumkamata. Hata hivyo, sababu ya kukamatwa kwake bado haijafahamika wazi, na haijathibitishwa ikiwa ana uhusiano wowote na shambulio la soko la Krismasi. Kuhusiana na tukio la soko la Krismasi, mshukiwa wa shambulio hilo ni daktari wa akili mwenye umri wa miaka 50, ambaye amekuwa akiishi Ujerumani kwa zaidi ya miaka 20. Inasemekana kuwa mtu huyo aliwahi kuwa Mwislamu lakini alibadili dini na kuonyesha misimamo mikali dhidi ya Uislamu. Tukio hili limeibua maswali kuhusu uhuru wa kujieleza kidini na namna mamlaka za Ujerumani zinavyoshughulikia matuk...

SWITZERLAND KUANZA KUITEKELEZA SHERIA YA KUPIGA MARUFUKU UVAJI WA NIKABU MWAKA 2025

Image
Serikali ya Switzerland Disemba 21, 2024 imepitisha sheria mpya ya kupiga marufuku kufunika uso hadharani nchini Uswizi, inayojulikana kama “burqa ban,” itaanza kutekelezwa rasmi kuanzia Januari 1, 2025. VIWANGO VYA ADHABU Wanaokiuka sheria hii watatozwa faini ya hadi 1,000 Francs za Kiswizi (takriban Dola za Marekani 1,144). SHERIA NA VIZUIZI Marufuku haya yatakuwa na msamaha katika mazingira maalum, ikiwa ni pamoja na: • Maeneo ya kidini au ibada. • Sababu za kiafya na usalama. • Hali ya hewa ya baridi kali. • Sherehe za kitamaduni au maonesho ya kisanii. HISTORIA YA SHERIA HII Sheria hii ilipitishwa na kura ya maoni mwaka 2021, ambapo asilimia 51.2 ya wapiga kura waliunga mkono marufuku hiyo. MAONI TOFAUTI Wakati wafuasi wa sheria wakisisitiza kuwa inalenga kulinda usalama wa umma na kuimarisha maadili ya kijamii, wakosoaji wanadai kuwa sheria hiyo inalenga kuwakandamiza wanawake wa Kiislamu wanaovaa burqa au niqab, hivyo kukiuka uhuru wa kidini na haki za binadamu. ...

MKESHA USIOSAHAULIKA LIVE WA ARISE & SHINE KAWE

Image
Mkesha usiosahaulika wa Arise & Shine Kawe ni tukio la kipekee linalolenga kuwaleta watu pamoja kwa ajili ya kumshukuru Mungu, kufanyika maombi, na kuimarisha maisha ya kiroho. Tukio hili linaendelezwa na kanisa/madhabahu ya Arise & Shine Kawe, likihusisha: 1. Ibada ya Sifa na Kuabudu: Usiku mzima wa kumtukuza Mungu kupitia nyimbo za kiroho na maombi ya nguvu. 2. Mafundisho ya Neno la Mungu: Wahubiri wa kipekee na wenye mafuta watakuwepo kuhubiri neno lenye kubadilisha maisha. 3. Maombi ya Kipekee: Maombi ya uponyaji, maombi ya kuombea familia, taifa, na mafanikio binafsi. 4. Shuhuda: Washiriki  wametoa shuhuda za  matendo makuu ya Mungu katika maisha yao. 5. Burudani za Kikristo: Kumekuwa na waimbaji wa Injili maarufu ambao watakuwepo kuleta burudani ya kiroho. Kanisa la Arise & Shine linapatikana Kawe Dar es salaam Kuanzia saa 12 jioni Disemba 13, 2024 hadi alfajiri Disemba 14, 2024 bure, lakini mshiriki anatakiwa kuja na moyo wa kumtafuta Mun...

MANENO YA PAPA FRANCIS KUHUSU YANAYOENDELEA UKRAINE NA RUSIA

Image
  KAULI YA PAPA FRANCIS DHIDI YA UKRAINE NA RUSIA  Kufuatia vitendo vya kuashiria vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema hatari ya vita ilmesababisha maumivu makali moyoni mwake. Ametoa wito kwa watu wote kutumia siku ya Machi 2, 2022 ambayo ni Jumatano ya Majivu, kufunga na kuiombea Ukraine. Ripoti zinaonesha tayari Russia imeanza kuishambulia Ukraine. Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amesema watashinda vita hiyo. Nukuu ya papa  “Call to prayer and fasting requested by Pope Francis for March 2, 2022  Pope Francis: "I have great pain in my heart over the worsening situation in Ukraine," "I would like all those who have the political responsibility to make a serious examination of conscience before God, who is the God of peace and not of war... He wants us to be brothers and not enemies. I pray that all parties involved will refrain from any action that will cause even more s...