BIASHARA KARIAKOO KUFANYIKA SAA 24 UZINDUZI FEBRUARI 22,2025
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametangaza kuwa biashara katika Soko la Kariakoo zitaanza kufanyika saa 24. Uzinduzi rasmi wa mfumo huo utafanyika Februari 22, ukianzia katika ofisi za Mkuu wa Mkoa hadi Kariakoo. RC Chalamila amesema hatua hii inalenga kuongeza fursa za kiuchumi, kuboresha mazingira ya biashara, na kuhakikisha wafanyabiashara wanapata muda wa kutosha kuhudumia wateja wao bila vikwazo vya muda. Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa biashara na usalama imejipanga kuhakikisha mazingira yanakuwa salama kwa wafanyabiashara na wateja katika kipindi chote cha biashara saa 24. Taarifa zaidi kuhusu utaratibu wa utekelezaji wa mfumo huu zitaendelea kutolewa kwa umma.