Posts

Showing posts with the label Kumbukizi

MKUU WA MAJESHI ATANGAZA KIFO CHA MEJA JENERALI MARTIN BUSUNGU (MSTAAFU)

Image
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, ametangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Meja Jenerali Martin Shiminzi Busungu (Mstaafu) ambaye  amefariki dunia tarehe 24 Desemba 2024, majira ya saa 10:15 jioni, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Enzi za utumishi wake, Meja Jenerali Busungu alishikilia nyadhifa mbalimbali muhimu, zikiwemo: • Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT): Aliongoza kuanzia mwaka 2018 hadi 2019. • Mkuu wa Jeshi la Akiba (Mgambo): Alihudumu kuanzia mwaka 2019 baada ya kuhama kutoka JKT. Wakati wa uongozi wake, alisimamia miradi mingi ya maendeleo, ikiwemo uzinduzi wa Kiwanda cha Kuchakata Mahindi cha Mlale JKT huko Songea, mkoani Ruvuma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, ratiba ya utoaji wa heshima za mwisho na mazishi ya marehemu itatangazwa baadaye. Mungu ailaze roho ya Meja Jenerali Busung...

HERI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU WA TANZANIA

Image
KAULI MBIU: “UONGOZI MADHUBUTI NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NI MSINGI WA MAENDELEO YETU” 1961 - 2024 Leo tunasherehekea miaka 63 tangu Tanzania ilipopata uhuru wake kutoka kwa wakoloni. Tarehe 9 Desemba 1961, Tanganyika, chini ya uongozi thabiti wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ilijipatia uhuru kupitia juhudi za kisiasa, mshikamano wa wananchi, na mazungumzo ya amani. Kupata uhuru hakukuwa kazi rahisi. Kulihitajika juhudi kubwa kupitia vyama vya kisiasa kama TANU (Tanganyika African National Union), ambavyo viliongoza mapambano ya kupigania haki za wananchi na kusimamia azma ya kujitawala. Kwa miaka 63, tumedumisha amani, mshikamano, na maendeleo ya taifa. Kauli mbiu ya mwaka huu inatukumbusha kwamba uongozi bora na ushirikiano wa wananchi ndiyo nguzo kuu ya mafanikio yetu. Tushirikiane kuendeleza urithi wa uhuru wetu kwa kujenga taifa lenye haki, umoja, na maendeleo. Hongera Tanzania!