MKUU WA MAJESHI ATANGAZA KIFO CHA MEJA JENERALI MARTIN BUSUNGU (MSTAAFU)


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, ametangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Meja Jenerali Martin Shiminzi Busungu (Mstaafu) ambaye  amefariki dunia tarehe 24 Desemba 2024, majira ya saa 10:15 jioni, wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.


Enzi za utumishi wake, Meja Jenerali Busungu alishikilia nyadhifa mbalimbali muhimu, zikiwemo:

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT): Aliongoza kuanzia mwaka 2018 hadi 2019.

Mkuu wa Jeshi la Akiba (Mgambo): Alihudumu kuanzia mwaka 2019 baada ya kuhama kutoka JKT.


Wakati wa uongozi wake, alisimamia miradi mingi ya maendeleo, ikiwemo uzinduzi wa Kiwanda cha Kuchakata Mahindi cha Mlale JKT huko Songea, mkoani Ruvuma.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kanali Gaudentius Gervas Ilonda, ratiba ya utoaji wa heshima za mwisho na mazishi ya marehemu itatangazwa baadaye.


Mungu ailaze roho ya Meja Jenerali Busungu mahali pema peponi. Amina.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA