Posts

Showing posts with the label Elimika

MAMA WA ELON MUSK, MAYE MUSK, AONYESHA KUSIFIA MTINDO WA MAISHA YA AFYA NA USHAWISHI WAKE DUNIANI

Image
Maye Musk, mama wa Elon Musk, ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika tasnia ya mitindo na umaarufu duniani kote. Katika mahojiano ya hivi karibuni, alielezea jinsi alivyokutana na mumewe, Errol Musk, akisema alikutana naye akiwa na umri wa miaka 15 na walikuwa na familia ya furaha kabla ya changamoto za kifamilia kuathiri ndoa yao. Pia, alizungumzia malezi ya watoto wake, akisisitiza umuhimu wa kuwafundisha kujitegemea na kuwapa uhuru wa kuchagua njia zao maishani. Mama wa Elon Musk, Maye Musk, amejiweka kuwa mfano wa kuigwa katika afya na ustawi, akiwa na umri wa miaka zaidi ya 80 na akiwa na umbo la kuvutia. Ametaja mara kadhaa jinsi anavyoshikilia mtindo wa maisha wa lishe bora na mazoezi ili kubaki na afya nzuri. Maye Musk anasema kuwa siri ya kuzeeka kwa afya ni pamoja na kula vyakula vya asili na kuepuka vyakula vilivyotengenezwa kwa viwanda. Yeye hupendelea: 1. Matunda na Mboga: Maye anasisitiza kula matunda na mboga za kijani kila siku, kwani ni chanzo kizuri cha vitami...

BOXING DAY:ASILI NA MAANA

Image
Boxing Day, ambayo huadhimishwa kila Desemba 26, ni siku ya mapumziko na utoaji zawadi katika nchi nyingi za Jumuiya ya Madola, kama Uingereza, Canada, Australia, na Afrika Kusini. Asili ya Jina “Boxing Day” 1. Sanduku la Zawadi (Christmas Boxes): Katika karne ya 19, wafanyakazi walipokea “sanduku za Krismasi” kutoka kwa waajiri wao siku baada ya Krismasi, zikiwa na zawadi, pesa, au vyakula kama shukrani kwa kazi yao mwaka mzima. 2. Misaada kwa Masikini: Siku hii pia ilihusishwa na makanisa kufungua “sanduku za sadaka” zilizokusanywa kwa ajili ya maskini na wahitaji. Shughuli za Boxing Day • Michezo: Siku hii hujulikana kwa mechi za soka nchini Uingereza na michezo mingine katika nchi za Jumuiya ya Madola. • Manunuzi: Katika nchi kama Canada, Australia, na Uingereza, Boxing Day imekuwa maarufu kwa mauzo makubwa madukani, sawa na Black Friday. • Ukarimu: Watu hutoa misaada kwa wahitaji au kutumia muda na familia na marafiki kwa chakula cha pamoja au ...

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA YAWAFIKIA WAFUNGWA GEREZA KUU ARUSHA

Image
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ametangaza kuwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, maarufu kama Mama Samia Legal Aid Campaign, inalenga kupunguza msongamano wa wafungwa na mahabusu magerezani. Akiwa katika ziara ya kikazi katika Gereza Kuu la Kisongo, jijini Arusha, Desemba 18, 2024, Waziri Ndumbaro amezungumza na wafungwa wa kike na kiume ili kusikiliza changamoto zao katika kupata msaada wa kisheria. Changamoto Magerezani Waziri Ndumbaro ameeleza  kuwa msongamano magerezani unatokana na changamoto katika mfumo wa haki jinai, ikiwemo watu kuhukumiwa kwa kushindwa kujitetea au kwa kusingiziwa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameanzisha kampeni hiyo kusaidia wahitaji kupata msaada wa kisheria, ambao utachangia kupunguza msongamano magerezani kwa kuhakikisha haki inatendeka. “Tunaangalia mfumo wa haki jinai kupitia taasisi zetu ili zifungamane na taasisi za magereza kwa lengo la kusaidia wafungwa na mahabusu kupa...

SHULE HII AUSTRALIA HURUHUSU WANAFUNZI KUVUTA SIGARA SHULENI

Image
Chuo cha Arethusa College, Queensland, Australia, kimezua mjadala kwa kuruhusu wanafunzi kuchukua mapumziko ya kuvuta sigara shuleni.  Taarifa zinaonyesha kuwa karibu wanafunzi 50 hutumia eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kuvuta sigara, hatua ambayo shule inadai husaidia kudhibiti uraibu wao na kuzuia athari mbaya kwa masomo yao. Uongozi wa shule unasema hatua hiyo inalenga kuzuia tabia hatarishi kama kuruka shule au kuvuta sigara kwa siri. Ingawa wanadai kupata kibali cha wazazi, baadhi ya wazazi wameonyesha wasiwasi, wakidai kuwa hatua hiyo imesababisha watoto wao kuanza kuvuta sigara. Arethusa College ni shule inayolenga wanafunzi waliotatizika katika mfumo wa kawaida wa elimu, lakini sera hii imeibua mjadala mkubwa kuhusu jukumu la shule katika malezi bora ya wanafunzi.

HATIMAE FURSA YA HATIFUNGANI YENYE FAIDA YAZINDULIWA

Image
Hatimae Hatifungani ya Miundombinu ya Barabara (Samia Infrastructure Bond) inaenda kuondoa changamoto ya  ucheleweshaji wa malipo ya Makandarasi kwa wakati wanapokuwa wamekamilisha kazi.  Hayo yameelezwa leo tarehe 29 Novemba, 2024 na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff wakati akitoa taarifa fupi katika hafla ya uzinduzi wa Hatifungani ya Miundombinu ya Barabara za Wilaya (Samia Infrastructure Bond) mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Isdory Mpango ambaye alimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Mhandisi Seff amebainisha kuwa kuanzishwa kwa Hatifungani hiyo ni muendelezo wa utatuzi wa changamoto wanazokabiliana nazo wakati wa utekelezaji wa jukumu la usimamizi, ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya barabara za wilaya zenye urefu wa Kilomita 144,429.77 ikiwa ni pamoja na madaraja 3,560 pamoja na makalavati 80,326. "Changamoto kubwa tuliyo...

HAKIKI NAMBA YAKO KUNA NIDA ZIMESAJILI NAMBA ZA WAHALIFU

Image
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa amewataka Wananchi kuhakiki namba zao za simu walizosajili katika vitambulisho vyao vya Nida ili kuepuka wahalifu kuzitumia. Kadhalika Waziri Silaa amewataka wananchi kutumia namba 100 kupata huduma za simu na si vinginevyo.

HIZI NDIZO SABABU ZINAZOKUFANYA ULIPIE UMEME KWA GHARAMA KUBWA

Image
  Unaweza kushangaa kuona wengine wakinunua Umeme wa 9,150 Wanapata Unit 75 wew ukinunua Umeme wa 10,000 unapata Unit 28.1 Iko hivi Watumiaji wadogo wa Umeme ambao kwa mwezi Matumizi yao hayazidi Unit 75 Wapo Tarrif D1(4) Na wanauziwa Unit moja kwa Sh.122, Wakati watumiaji waliowengi wako Tarrif T1 hawa Unit moja wanauziwa Sh.kati ya sh.356.45 Kama sikosei Maana yake mtumiaji aliyeko Tarrif D1(4) Ananunua Unit 41 Kwa sh 5,000 Wakati walioko Tarrif T1 Wananunua Unit 14 kwa sh.5000 NAWEZAJE KUA MIONGONI MWA WATUMIAJI WADOGO WA UMEME YAANI (TARIFF D1) Kama ni nyumba yakupanga na mko wengi ni ngumu kidogo. Kwanza unatakiwa Kupunguza Matumizi Ya Umeme Yasiyo ya Lazima Pili nunua Vifaa vyenye Wats ndogo vitu kama taa,Tv,Friji,Pasi n.k Tuchukulie mfano wa Taa zenye Wats 40 nje zikiwa nne na za Wats 18 kwa ndani zikawa Taa 8 nyumba yako nzima itakua na jumla ya Taa 12 Ambazo zitakua na Jumla ya Wats 304  Lakini ukinunua Taa zenye Wats ndogo (Energy Saver) Japo bei yake iko juu ukiling...