HIZI NDIZO SABABU ZINAZOKUFANYA ULIPIE UMEME KWA GHARAMA KUBWA

 


Unaweza kushangaa kuona wengine wakinunua Umeme wa 9,150 Wanapata Unit 75 wew ukinunua Umeme wa 10,000 unapata Unit 28.1

Iko hivi Watumiaji wadogo wa Umeme ambao kwa mwezi Matumizi yao hayazidi Unit 75 Wapo Tarrif D1(4) Na wanauziwa Unit moja kwa Sh.122,

Wakati watumiaji waliowengi wako Tarrif T1 hawa Unit moja wanauziwa Sh.kati ya sh.356.45 Kama sikosei

Maana yake mtumiaji aliyeko Tarrif D1(4) Ananunua Unit 41 Kwa sh 5,000

Wakati walioko Tarrif T1 Wananunua Unit 14 kwa sh.5000

NAWEZAJE KUA MIONGONI MWA WATUMIAJI WADOGO WA UMEME YAANI (TARIFF D1)

Kama ni nyumba yakupanga na mko wengi ni ngumu kidogo. Kwanza unatakiwa Kupunguza Matumizi Ya Umeme Yasiyo ya Lazima

Pili nunua Vifaa vyenye Wats ndogo vitu kama taa,Tv,Friji,Pasi n.k

Tuchukulie mfano wa Taa zenye Wats 40 nje zikiwa nne na za Wats 18 kwa ndani zikawa Taa 8 nyumba yako nzima itakua na jumla ya Taa 12 Ambazo zitakua na Jumla ya Wats 304 

Lakini ukinunua Taa zenye Wats ndogo (Energy Saver) Japo bei yake iko juu ukilinganisha na Taa zenye Wats kubwa Kwa mfano huu huu ukanunua Taa zenye Wats 5 kila moja za nje Nne na taa 8 za ndani zenye Wats 3 kila moja 

Jumla ya taa 12 zitakua na Jumla ya Wats 44 tu.

Maana yake utakua umepunguza jumla ya Wats 250 upande wa Taa tu lakini idadi ya Taa imeendelea kua ni ile ile. Mtu mwenye taa moja ya Wats 40 akiwasha nawew ukawa taa zote 12 Matumizi yenu yatakua hayana tofauti kubwa 

Ili kujua unatumia UNIT ngapi jumlisha watt za vifaa vyako vyote mfano vifaa vyako vyote vina idadi ya watt 100 ili utumie UNIT moja ni sawa na watt 100 kwa saa hivyo ukiwa na jumla ya watt 100 basi itakuwa ni sawa na masaa 10 ndo utumie unit 1 

Mwisho kabisha matumizi yako ya Umeme yakiwa chini ya Unit 75 kwa miezi mitatu mpaka Sita Mfululizo unatakiwa kuandika Barua unaiadress kwa Meneja wa TANESCO wa Ofisi uliyoko Karibu nayo Kuomba kubadilishiwa Kutoka Tarrif 1 kwenda Tarrif 4.

Siku ukitumia Zaidi ya Unit 75 kwa mwezi utarudishwa Tariff 1.


Kwa mahitaji ya ushauri na vifaa gani bora vya kutumia na upatikanaji wake  tutumie ujumbe 

Ahsanteni!

Tafadhali Usisahau kulike na kushare page hii

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA