Posts

Showing posts with the label Afya

TANZANIA YATEULIWA NA SOMALIA KUSHIRIKIANA KATIKA UGAVI WA BIDHAA ZA AFYA

Image
Wizara ya Afya nchini Somalia imeichagua Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kushirikiana kwenye masuala mbalimbali yanayohusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa kubadilishana uzoefu katika maeneo ya mifumo, ununuzi, usambazaji na udhibiti ubora. Hayo yamebainishwa na watendaji wa Wizara ya Afya kutoka Somalia waliotembelea Bohari ya Dawa (MSD), ambapo mwakilishi wa ugeni huo, Mohamed Abdulukadiri Hersi, ameeleza kuwa hatua mbalimbali zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia MSD katika mifumo ya ugavi inayotumia teknolojia ndio zimewavutia zaidi kuja kujifunza kwa kujionea namna inavyofanya kazi na kulinganisha na mifumo mingine ya serikali. Hersi ameongeza kuwa Somalia ipo kwenye mpango wa kujenga upya mfumo wake wa ugavi wa bidhaa za afya, ikiwa ni pamoja na kuboresha utaratibu wa kufikisha bidhaa za afya kwa wananchi. Amesema kati ya nchi walizozichagua kuwa mfano ni Tanzania, ambapo kupitia MSD wamejifunza mengi ambayo watakwenda kuyatekeleza watakaporudi. Naye Mkurugenz...

RAIS DKT. SAMIA KUANDIKA HISTORIA KWA KUPATA TUZO YA KIMATAIFA KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA AFYA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kupokea tuzo ya kimataifa ya The Gates Goalkeepers Award, ikiwa ni ishara ya kutambua mafanikio makubwa aliyoyapata katika uongozi wake, hususan katika kupunguza vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi. Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa Demografia na Afya ya mwaka 2022, Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya uzazi kwa asilimia 80, mafanikio yanayoifanya kuwa moja ya nchi zinazopiga hatua kubwa katika kuboresha afya ya mama na mtoto. Akizungumza jijini Dar es Salaam Februari 3, 2025, Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, alisema kuwa tukio hilo la utoaji wa tuzo linaloratibiwa na Taasisi ya The Gates Foundation litafanyika kwa mara ya kwanza nje ya Marekani, na Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji. Rais Samia Suluhu Hassan anakuwa kiongozi wa kwanza barani Afrika kupokea tuzo hiyo, hatua inayodhihirisha kutambuliwa kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya sekta ya afya na ustawi wa jamii. “Hii ni h...

SERIKALI YAZIDI KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA AKILI KWA KULETA MAPINDUZI KATIKA MAFUNZO NA AJIRA ZA WATAALAM

Image
Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa wataalam wa afya ya akili nchini kwa kuwajengea uwezo wataalam 2,980 kutoka vituo 710 vya afya kote nchini ili waweze kutoa huduma hizo kwa ufanisi katika maeneo yao. Hatua hii inalenga si tu kuongeza idadi ya wataalam waliobobea katika afya ya akili, bali pia kuhakikisha kuwa huduma hizo zinapatikana kwa urahisi katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya, hususan kwa wananchi walioko vijijini. Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Jesca Jonathani Msambatavangu, Bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, amesema kuwa Serikali inaendelea kupanua sekta ya afya ya akili kwa kuajiri wataalam zaidi na kuimarisha mafunzo kwa madaktari na wahudumu wa afya. “Kwa mwaka 2024 pekee, Serikali imeajiri jumla ya watumishi wapya 56 katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, ikiwa ni jitihada za kupunguza uhaba wa wataalam wa sekta hii muhimu,” alisema Dkt. Mollel. Katika...

MOI KUANZA USAJILI WA WAGONJWA KWA KUTUMIA NAMBA YA NIDA KUANZIA FEBRUARI 1

Image
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imetangaza kuwa kuanzia tarehe 1 Februari 2025, usajili wa wagonjwa utaanza kufanyika kwa kutumia namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA). Hatua hii inalenga kuboresha mfumo wa utambuzi wa wagonjwa, kuhakikisha upatikanaji wa taarifa zao kamili, na kuweka kumbukumbu sahihi kwa uboreshaji wa huduma za afya. Pia, itarahisisha usomaji na ubadilishanaji wa taarifa za mgonjwa kati ya taasisi mbalimbali za matibabu, kupunguza mkanganyiko wa taarifa, na kusaidia ndugu kumtambua mgonjwa endapo atashindwa kujitambulisha. Menejimenti ya MOI imewataka wagonjwa wote wanaofika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu kuhakikisha wanakuwa na Kitambulisho cha Taifa. Kwa wale ambao bado hawajapata kitambulisho hicho, watalazimika kuwasilisha barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa, Sheha, au Kijiji wanachoishi. Uwasilishaji wa barua hizo utafanyika hadi tarehe 30 Juni 2025. MOI inawahimiza wananchi kuchukua hatua mapema ili kuepusha usumbufu wakati...

ZAIDI YA ASILIMIA 97 YA WATU WAPATIWA DAWA ZA KINGATIBA YA MATENDE NA MABUSHA NCHINI

Image
 Serikali kupitia Wizara ya Afya imefanikiwa kuwapatia dawa za kingatiba ya matende na mabusha kwa wananchi 257,358 kati ya walengwa 265,217, sawa na asilimia 97, katika Halmashauri za Mtama na Mtwara Mikindani kwa mwaka 2024. Hatua hii ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kudhibiti na kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini. Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, ametoa takwimu hizo Januari 30, 2025, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Duniani. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Tuungane, Tuchukue Hatua, Tutokomeze Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele.” Kwa upande wa ugonjwa wa usubi, watu milioni 5,462,851 kati ya milioni 6,447,157 kutoka halmashauri 24 walipatiwa kingatiba, ikiwa ni sawa na asilimia 85 kwa mwaka 2024. Aidha, kuhusu ugonjwa wa trakoma, Waziri Mhagama amebainisha kuwa watu milioni 1,603,425 kati ya milioni 1,967,143 kutoka hadi halmashauri saba (Ngorongoro, ...

SERIKALI YAJIPANGA KIKAMILIFU KUKABILIANA NA MARBURG

Image
  Serikali inaendelea na juhudi za kudhibiti ugonjwa wa Marburg tangu ulipotangazwa kwa mara ya kwanza Januari 19, 2025, wilayani Biharamulo, mkoani Kagera. Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Dkt. Ntuli Kapologwe, alieleza Januari 24, 2025, kuwa wizara imeweka kambi wilayani humo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wahisiwa wa ugonjwa huo, sambamba na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kujikinga na kutambua dalili za ugonjwa huo. Mpaka sasa, idadi ya waliofariki ni wawili, wagonjwa wahisiwa ni 15, huku watu 281 waliokuwa karibu na waathirika wakiendelea kufuatiliwa. “Serikali imeimarisha udhibiti wa ugonjwa huu kwa kuleta madaktari bingwa, vifaa vya upimaji, madawa, pamoja na kuwashirikisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii, ambao wanapita nyumba kwa nyumba kubaini wahisiwa wa ugonjwa huo,” alisema Dkt. Kapologwe. Kwa mujibu wa Dkt. Kapologwe, wahudumu wa afya ngazi ya jamii 191 walioko kwenye mafunzo kwa vitendo wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za awali za matibabu kwa wananc...

HOSPITALI YA MUHIMBILI, JKCI, MOI, AGA KHAN ZAJIPANGA KUHUDUMIA WAGENI MKUTANO WA NISHATI

Image
  Hospitali ya Muhimbili, JKCI, MOI, na Aga Khan zimejipanga kutoa huduma bora kwa wageni watakaoshiriki Mkutano wa Nishati unaofanyika leo na kesho.  Mkutano huu, ambao unakusudia kukuza ufanisi na ubunifu katika sekta ya nishati, utahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu, viongozi serikalini, na wajasiriamali. Huduma zitakazotolewa ni pamoja na vipimo vya afya, ushauri wa kitabibu, na msaada wa haraka kwa wageni watakaohitaji huduma za dharura. Hospitali hizi zimeandaa timu maalum ya wahudumu na vifaa vya kisasa kuhakikisha kuwa huduma za afya zipo kwa wepesi na ufanisi.

WAZIRI WA AFYA APONGEZA USHIRIKIANO WA TANZANIA NA CHINA, APOKEA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA TZS MILIONI 125

Image
  Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, amepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya TZS Milioni 125 kutoka Serikali ya Watu wa China. Msaada huu unalenga kuboresha huduma za afya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kukabiliana na changamoto za utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Katika hafla ya makabidhiano, Mhe. Mhagama amesema msaada huo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na China. Alibainisha kuwa ushirikiano huu unazidi kuimarika kupitia maboresho ya huduma za afya, upatikanaji wa wataalamu mabingwa na vifaa vya kisasa vya teknolojia ya hali ya juu. “Naupongeza uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kusimamia vyema ushirikiano huu. Msaada huu utachochea maendeleo katika sekta ya afya na kuleta matokeo bora kwa wananchi,” alisema Mhe. Mhagama. Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, aliishukuru Wizara ya Afya na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana kwa karibu na madaktari wa China waliopo nch...

MARBURG YATISHA: MMOJA AFARIKI, MMOJA HOSPITALINI, 281 WAFUATILIWA

Image
Serikali ya Tanzania imethibitisha mlipuko mpya wa ugonjwa wa Marburg katika mkoa wa Kagera. Mlipuko huu unahusisha kifo cha mtu mmoja, mgonjwa mmoja aliye hospitalini, na watu 281 wanaofuatiliwa baada ya kugusana na mgonjwa aliyethibitika kuwa na virusi hivyo. Marburg, ugonjwa unaofanana na Ebola, husababisha homa kali, maumivu ya kichwa, udhaifu, na mara nyingine kuvuja damu. Ugonjwa huu ni hatari sana, ukiwa na kiwango cha vifo kinachofikia asilimia 90 katika baadhi ya milipuko. Taasisi ya afya nchini, kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), imeanza hatua za kudhibiti maambukizi ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa mawasiliano, elimu kwa umma, na utoaji wa msaada wa matibabu. Mlipuko huu unafuatia ule wa Machi 2023, ambapo kulikuwa na visa tisa na vifo sita katika mkoa huo huo wa Kagera. Serikali imewataka wananchi kuchukua tahadhari, kuripoti dalili za ugonjwa, na kuepuka kugusana na watu wenye dalili za Marburg.  

WIZARA YA AFYA YATOA MWONGOZO KWA WASAFIRI KUFUATIA MLIPUKO WA UGONJWA WA MARBURG

Image
 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Afya, imetangaza Mwongozo Na. 15 wa tarehe 21 Januari 2025 baada ya kuthibitisha mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi vya Marburg (MVD) katika Wilaya ya Biharamulo, Mkoa wa Kagera. Wilaya hiyo ipo umbali wa kilomita 1,450 kutoka Dar es Salaam na kilomita 1,068 kutoka Arusha. Katibu Mkuu Wizara ya afya  Dkt. Seif A. Shekalagne amesema Mwongozo huu unalenga kuchukua hatua za haraka na madhubuti ili kudhibiti mlipuko na kuzuia usambazaji wa ugonjwa huo ndani na nje ya nchi, kwa kuzingatia Kanuni za Afya za Kimataifa za mwaka 2005. HATUA ZA KUDHIBITI NA KUZUIA USAFIRI: 1. Fomu za Ufuatiliaji Wasafiri wote wanaotoka Mkoa wa Kagera wanatakiwa kujaza fomu ya ufuatiliaji wa wasafiri kupitia mtandao kwa anuani https://afyamsafiri.moh.go.tz. 2. Ufuatiliaji wa Waliokaribu na Wagonjwa Watu wote waliokuwa karibu na mgonjwa wa Marburg watafuatiliwa kwa ukaribu na hawataruhusiwa kutoka maeneo ya kujitenga hadi wapate kibali rasm...

DKT. SAMIA ATANGAZA KESI MOJA YA VIRUSI VYA MARBURG

Image
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametangaza kubainika kwa mgonjwa mmoja aliyeambukizwa virusi vya Marburg (MVD) katika Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera. Rais Samia alizungumza mjini Dodoma katika mkutano wa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambapo alithibitisha kuwa kisa hicho kimepata uthibitisho baada ya vipimo vya kitaalamu kufanywa katika Maabara ya Kabaile na kuthibitishwa jijini Dar es Salaam. Wiki iliyopita, Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, alikanusha taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa Marburg nchini, akisema hakuna mtu aliyepatikana na maambukizi ya virusi hivyo. Hata hivyo, Rais Samia amesema hii sio mara ya kwanza kwa Tanzania kukumbwa na mripuko wa Marburg, kwani ugonjwa huo ulianza kuibuka kwa mara ya kwanza Machi 2023 katika mkoa wa Kagera. Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kudhibiti maambukizi na kuhakikisha usalama wa wananchi, huku wananchi wakitakiwa kufuata maelekezo ya...

MADAKTARI BINGWA WATOA HUDUMA KWA WANANCHI ZAIDI YA 2,000 TEMEKE

Image
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke, Dkt. Joseph Kimaro, amesema kuwa zaidi ya wananchi 2,000 wamepata matibabu ya kibingwa katika kambi maalumu ya siku tano iliyofanyika hospitalini hapo. “Wakati wa kambi hii maalumu, tumewahudumia jumla ya wagonjwa 2,442. Kati yao, wanawake walikuwa 1,478, sawa na asilimia 61, huku wanaume wakiwa 964, sawa na asilimia 39. Pia, watoto chini ya miaka mitano waliohudumiwa walikuwa 282,” alisema Dkt. Kimaro. Aidha, Dkt. Kimaro alieleza kuwa kambi hiyo imebaini kuwa asilimia 63 ya wagonjwa waliohudumiwa walikuwa na magonjwa yasiyoambukiza, jumla yao ikiwa 1,538. “Madaktari Bingwa 55 walihusika katika kutoa huduma mbalimbali za kibingwa, ikiwemo upasuaji kwa wagonjwa 59. Upande wa maabara ulifanya vipimo 1,861, huku huduma za radiolojia zikijumuisha vipimo 702, ikiwemo Ultrasound, CT Scan na X-ray,” aliongeza. Kwa upande wake, Dkt. Bryceson Kiwelu, mmoja wa Madaktari Bingwa, aliwahimiza wananchi kuzingatia mtindo bora wa ...

DCEA YATEKETEZA KILO 185 ZA ‘UNGA’

Image
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini, kwa niaba ya Kamishna Jenerali, January 16, 2025 imeteketeza jumla ya kilo 185.35 za dawa za kulevya aina ya ‘unga’. Uteketezaji huo ulifanyika katika Dampo la Maji ya Chai lililopo wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha, na ni sehemu ya juhudi kubwa za kupambana na matumizi ya dawa za kulevya nchini. Aidha, DCEA iliteketeza kilo 154.35 za mirungi na kilo 31 za bangi mbichi. Jumla ya watuhumiwa watano walikamatwa kwa makosa ya kupatikana na dawa hizo. Uteketezaji huu ulifanyika kwa kuzingatia taratibu za kisheria, na mahakama ya Wilaya ya Arumeru iliridhia uchomaji wa vielelezo hivyo kwa kuwa dawa hizo zinaweza kuwa hatari kwa afya ya binadamu endapo zitaendelea kuhifadhiwa. Mkuu wa Oparesheni kutoka DCEA Kanda ya Kaskazini, Innocent Masangula, alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na mamlaka katika kupambana na dawa za kulevya. Aidha, Ofisa Sheria wa DCEA, Benson Mwaitenda, alisisitiza kuwa sheria dhidi ya dawa ...

WAZIRI WA AFYA ATEUA NA KUZINDUA BARAZA LA UUGUZI NA UKUNGA TANZANIA (TNMC) ASISITIZA UZALENDO KATIKA KUFANYA MAAMUZI

Image
Waziri wa Afya Mhe. Jenesta Mhagama (Mbunge) amefanya uteuzi na kuzindua Baraza jipya la Uuguzi na Ukunga Tanzania(TNMC) lenye jumla ya    wajumbe 12 baada ya wajumbe wa Baraza la awali kumaliza muda wao. Uteuzi wa wajumbe 12 wa Baraza ni kwa Mujibu wa kifunga namba 5 - (1) cha Sheria iliyotungwa na Bunge ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 ambacho kimempa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Afya kufanya uteuzi wa wajumbe wa Baraza.   Akizungumzana katika hafla ya uzinduzi amewataka wajumbe hao kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Baraza kuhakikisha wanasimamia, wajibu, weledi na kudhibiti wanotaka kuvunja Sheria, kanuni na taratibu za sekta ya Afya kupitia taaluma ya Uuguzi na Ukunga. Kama serikali hatutamani kusikia muuguzi au Mkunga amavunja taratibu katika kutekeleza majukumu yake kwa sababu huyo mmoja anaharibu image ya wauguzi na wakunga wote, kwa hiyo mmepewa heshima ili ninyi mtusaidie na pale mtakapotakiwa kufanya dhidi ya wale wanaoharibu heshima na sifa ya taal...

TAARIFA KUHUSU HOFU YA VIRUSI VYA MARBURG MKOANI KAGERA

Image
  Serikali imethibitisha uwepo wa hofu ya mlipuko wa ugonjwa unaoshukiwa kuwa virusi vya Marburg katika mkoa wa Kagera Januari 15, 2025 kufuatia taarifa za watu wanane kufariki dunia. Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti tukio hilo na kuelezea kuwa uchunguzi unaendelea kuthibitisha sababu halisi za vifo hivyo. Serikali imesisitiza kuwa juhudi zimeimarishwa kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na: • Kuongeza kasi ya uchunguzi wa kiafya kwa wagonjwa. • Kuimarisha ufuatiliaji wa watu waliokutana na wagonjwa wanaoshukiwa. • Kupeleka wataalamu wa afya na vifaa vya dharura mkoani Kagera. Wananchi wanashauriwa kuchukua tahadhari zote za kiafya, ikiwemo kujiepusha na mawasiliano ya karibu na wagonjwa au maiti zinazohusishwa na dalili za Marburg. Pia, taarifa za mara kwa mara zitakuwa zikitolewa na mamlaka husika.

HUDUMA ZA DHARURA NJE YA HOSPITALI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU KUIMARISHWA

Image
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kutekeleza mkakati wa kuimarisha huduma za dharura nje ya hospitali kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi. Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu, alipotembelea kampuni ya Emergency Medical Services inayofahamika kama E-Plus Tanzania, iliyoko Mikocheni, Dar es Salaam. Kampuni hiyo ni miongoni mwa watoa huduma za ambulance nchini. Dkt. Jingu alisema kuwa E-Plus imekuwa mshirika muhimu wa Serikali katika kuhakikisha huduma za dharura zinapatikana kwa wakati na kwa ubora unaohitajika. “Nimewasikiliza na kupokea maoni yao kuhusu maeneo ambayo wanahitaji msaada kutoka Serikalini ili kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Kwa mujibu wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Serikali ina jukumu la kuwezesha sekta binafsi ili iweze kuchangia kikamilifu maendeleo ya huduma za afya, hususan huduma za dharura,” alisema Dkt. Jingu. HUDUMA BORA ZA DHARURA Katika ziara hiyo, Dkt. Jingu alitem...

SERIKALI KUJA NA MIFUMO YA HUDUMA ZA DHARURA RAFIKI NA WEZESHI KWA WATUMIAJI

Image
Na WAF, Dar es Salaam Serikali inaendelea kuimarisha mifumo ya huduma za dharura kwa kuanzisha mifumo ya mawasiliano ya kidigitali katika hospitali ya Taifa Muhimbili na nyinginezo nchini, ili kutoa huduma rafiki na wezeshi kwa watumiaji na kufikia lengo la kuokoa maisha. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu, Januari 9, 2025, Jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Mradi wa Kuimarisha Huduma za Matibabu ya Dharura katika hospitali ya Muhimbili. Dkt. Jingu alisema kuwa huduma za dharura ni muhimu kwa ustawi wa jamii, hasa katika kuokoa maisha pale zinapotokea changamoto kama ajali au magonjwa ya ghafla. “Huduma za Dharura haziishii kwenye Ambulance tu, tunataka mtu anayepata dharura apokee huduma haraka na kwa ufanisi. Mfumo wa mawasiliano unahitaji kuimarika ili kuboresha matibabu ya dharura,” alisema Dkt. Jingu. Amesisitiza kuwa, Serikali inaendelea kuboresha mifumo hiyo, na ni muhimu kuhakikisha vifaa vya dharura, ikiwa ni pamoja na magari ya w...

MILIONI 600 KUIPANDISHA HADHI ZAHANATI YA SUJI KUWA KITUO CHA AFYA

Image
Na WAF - Same, Kilimanjaro Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi Milioni 600 kwa ajili ya kuipandisha hadhi Zahanati ya Suji iliyopo Kijiji cha Malindi, Wilaya ya Same, Kilimanjaro kuwa Kituo cha Afya. Hatua hii inalenga kuongeza huduma za afya, ikiwemo huduma za kulaza wagonjwa na chumba cha upasuaji wa dharura. Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, alitoa taarifa hiyo tarehe 8 Januari 2025, alipokuwa akikagua na kuzindua miradi ya afya mkoani Kilimanjaro. Alisema kuwa hatua ya kuipandisha hadhi zahanati hiyo itahakikisha wananchi wanapata huduma za afya karibu na maeneo yao. “Ni muhimu tukaongeza huduma za afya Suji kwa kuwa na wodi maalum za kulaza wagonjwa, chumba cha upasuaji, na huduma za mionzi. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha dhamira kubwa kwa kuleta maendeleo haya kupitia usimamizi bora wa rasilimali,” alisema Waziri Mhagama. Zahanati ya Suji inahudumia wananchi wanaokabiliwa na changamoto ya kusafiri zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma za afya, ikiwemo hu...

WAZIRI MHAGAMA ATEKELEZA MAAGIZO YA MAKAMU WA RAIS UJENZI WA CHUO CHA WAUGUZI

Image
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama ametekeleza kwa vitendo maagizo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ya ujenzi wa chuo cha wauguzi kitakachojengwa pembeni ya hospitali ya wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.  Waziri Mhagama amesema hayo leo Januari 7, 2024 akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kukagua na kuzindua miradi ya sekta mbalimbali ikiwemo ya sekta ya afya katika Wilaya ya Rombo pamoja na wilaya ya Same ambapo leo amezindua wodi ya wazazi iliyopo katika kituo cha afya Mkuu - Rombo.  "Ndugu zangu Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haijawahi kupoa, hasa kwenye sekta ya afya, tupo macho kupokea maelekezo na kuyatekeleza, sasa ujenzi wa chuo chetu cha wauguzi utaanza mwezi wa tatu, ili kupunguza tatizo la watumishi ndani ya wilaya, mkoani na Tanzania kwa ujumla," amesema Waziri Mhagama. Waziri Mhagama amesema tayari Wizara ya Afya imetenga Shilingi Bilioni Moja ili kuanza haraka iwezekanavyo uje...

KAMATI YA KANUNI YA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR NA ZHSF WAPONGEZA UBORESHAJI HUDUMA MUHIMBILI

Image
Wajumbe Kamati ya Kanuni na Sheria Ndogondogo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kufurahishwa na maboresho ya mifumo ya utoaji huduma ikiwemo miundombinu, mazingira ya utoaji huduma zenyewe pamoja na uwekezaji wa vifaa tiba. Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mihayo Juma Nungu amesema baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hospitali wameona maboresho mengi na kujifunza namna ambavyo wataenda kuyatekeleza ili kuboresha zaidi utoaji huduma za kibingwa na ubingwa bobezi huko Zanzibar. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya ZHSF Mhe. Mbarouk Omar Mohammed amesema wameona namna ambavyo wanachama wa Mfuko wa Taifa Bima ya Afya NHIF yenye uzoefu wa karibu miaka 25 na ZHSF yenye uzoefu wa zaidi ya mwaka mmoja wanavyohudumiwa hospitali hapo na kuongeza kuwa utoaji huduma unaenda vizuri na pale penye changamoto zinatatuliwa kwa wak...