WAZIRI WA AFYA ATEUA NA KUZINDUA BARAZA LA UUGUZI NA UKUNGA TANZANIA (TNMC) ASISITIZA UZALENDO KATIKA KUFANYA MAAMUZI


Waziri wa Afya Mhe. Jenesta Mhagama (Mbunge) amefanya uteuzi na kuzindua Baraza jipya la Uuguzi na Ukunga Tanzania(TNMC) lenye jumla ya    wajumbe 12 baada ya wajumbe wa Baraza la awali kumaliza muda wao.


Uteuzi wa wajumbe 12 wa Baraza ni kwa Mujibu wa kifunga namba 5 - (1) cha Sheria iliyotungwa na Bunge ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 ambacho kimempa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Afya kufanya uteuzi wa wajumbe wa Baraza. 


 Akizungumzana katika hafla ya uzinduzi amewataka wajumbe hao kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Baraza kuhakikisha wanasimamia, wajibu, weledi na kudhibiti wanotaka kuvunja Sheria, kanuni na taratibu za sekta ya Afya kupitia taaluma ya Uuguzi na Ukunga.


Kama serikali hatutamani kusikia muuguzi au Mkunga amavunja taratibu katika kutekeleza majukumu yake kwa sababu huyo mmoja anaharibu image ya wauguzi na wakunga wote, kwa hiyo mmepewa heshima ili ninyi mtusaidie na pale mtakapotakiwa kufanya dhidi ya wale wanaoharibu heshima na sifa ya taaluma yetu, muongozwe na uzalendo kwa maslahi ya jamii nzima ya Watanzania.

wajumbe wapya watahudumu kwa kipindi kisichozidi miaka mitatu tangu kuteuliwa kwao.



 

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA