RAIS SAMIA AZINDUA SERA MPYA YA ELIMU, AZITAKA WIZARA HUSIKA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WAKE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa uwepo wa Sera Mpya ya Elimu na Mitaala Mipya pekee haviwezi kuleta matokeo chanya bila utekelezaji makini. Akizungumza Februari 1, 2025, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 – Toleo la 2023, Rais Samia ameagiza wizara husika kuhakikisha kuwa utekelezaji wa sera hiyo unafanyika kikamilifu ili kuleta matokeo yaliyokusudiwa. “Naitaka Wizara ya Fedha, Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, pamoja na TAMISEMI kuwezesha na kusimamia utekelezaji wa sera na mitaala hii mpya kwa ufanisi,” amesema Rais Samia. MAGEUZI KATIKA SEKTA YA ELIMU Katika hotuba yake, Rais Samia amesisitiza kuwa maboresho hayo lazima yawazingatie walimu kwa kuwapatia mafunzo sahihi, kuwaajiri wenye sifa stahiki, na kuboresha maslahi yao. Aidha, ameweka wazi kuwa dhamira ya mabadiliko haya ni kumuandaa kijana mwenye kujiamini na aliye tayari kushindana katika soko la...