WAVULANA WAONGOZA UFAULU KIDATO CHA NNE, WANAFUNZI 450 KURUDIA MITIHANI 2025


 

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne wa mwaka 2024, ambapo asilimia 92.37 ya watahiniwa wamefaulu. Hii ni ongezeko la ufaulu kwa asilimia 3 ikilinganishwa na mwaka 2023, ambao ulikuwa na ufaulu wa asilimia 89.36.


Katika matokeo haya, jumla ya watahiniwa 477,262 kati ya 516,695 waliofanya mtihani huo wamepata madaraja ya I, II, III, na IV. Kwa upande wa jinsia, wasichana wameongoza kwa idadi ya waliofaulu, wakiwa ni 249,078 sawa na asilimia 52, huku wavulana wakiwa ni 228,184 sawa na asilimia 48.


Hata hivyo, wavulana wameongoza kwa ubora wa ufaulu, ambapo asilimia 54 ya waliofaulu kwa madaraja ya I hadi III ni wavulana (119,869), ikilinganishwa na asilimia 46 ya wasichana (102,084).


Aidha, NECTA imetangaza kuwa wanafunzi 450 ambao matokeo yao yamezuiwa kwa sababu mbalimbali, ikiwemo udanganyifu na changamoto nyingine, wamepewa fursa ya kurudia mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2025.


NECTA imetoa wito kwa wanafunzi waliokosa ufaulu wa viwango bora kutumia vyema nafasi ya kurudia mtihani ili kuboresha matokeo yao na kufikia malengo yao ya kitaaluma.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA