DKT. SAMIA AWATAKIA KHERI WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 11 Novemba 2024, amewatakia kila la kheri wanafunzi wote wa Kidato cha Nne wanapoanza Mtihani wa Kuhitimu (CSEE) leo.
Aidha Dkt. Samia kupitia mtandao wake wa X anawaombea utulivu na mafaniko katika hatua hii muhimu ya watahiniwa wote kujiandaa kushiriki vyema kwenye nguvu kazi ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
"Mafanikio yenu katika hatua hii yatakuwa pia faraja kwa waalimu, wazazi na Watanzania wote ambao kupitia ulipaji kodi na utunzaji wa amani na utulivu wa nchi yetu mnaiwezesha Serikali kuendelea kutekeleza mipango tunayojiwekea, ikiwemo kutoa elimu bure kuanzia Darasa la Kwanza hadi Kidato cha Sita, na kazi mpya tuliyoanza ya kuboresha mfumo wetu wa elimu ili uendane na mazingira na mahitaji ya sasa.
Mwenyezi Mungu awaongoze na kuwasimamia." ameandika

Comments