TANZANIA YATEULIWA NA SOMALIA KUSHIRIKIANA KATIKA UGAVI WA BIDHAA ZA AFYA


Wizara ya Afya nchini Somalia imeichagua Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kushirikiana kwenye masuala mbalimbali yanayohusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa kubadilishana uzoefu katika maeneo ya mifumo, ununuzi, usambazaji na udhibiti ubora.


Hayo yamebainishwa na watendaji wa Wizara ya Afya kutoka Somalia waliotembelea Bohari ya Dawa (MSD), ambapo mwakilishi wa ugeni huo, Mohamed Abdulukadiri Hersi, ameeleza kuwa hatua mbalimbali zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia MSD katika mifumo ya ugavi inayotumia teknolojia ndio zimewavutia zaidi kuja kujifunza kwa kujionea namna inavyofanya kazi na kulinganisha na mifumo mingine ya serikali.


Hersi ameongeza kuwa Somalia ipo kwenye mpango wa kujenga upya mfumo wake wa ugavi wa bidhaa za afya, ikiwa ni pamoja na kuboresha utaratibu wa kufikisha bidhaa za afya kwa wananchi. Amesema kati ya nchi walizozichagua kuwa mfano ni Tanzania, ambapo kupitia MSD wamejifunza mengi ambayo watakwenda kuyatekeleza watakaporudi.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai, ameeleza kuwa wageni hao wamekuja Tanzania kwa muda muafaka ambapo MSD imefanya mageuzi makubwa ya kiutendaji, ikiwemo kujiendesha kibiashara na kufanya maboresho mbalimbali katika mnyororo mzima wa ugavi wa bidhaa za afya, hivyo watajifunza mengi kupitia ziara hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA