TAARIFA KUHUSU HOFU YA VIRUSI VYA MARBURG MKOANI KAGERA
Serikali imethibitisha uwepo wa hofu ya mlipuko wa ugonjwa unaoshukiwa kuwa virusi vya Marburg katika mkoa wa Kagera Januari 15, 2025 kufuatia taarifa za watu wanane kufariki dunia. Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti tukio hilo na kuelezea kuwa uchunguzi unaendelea kuthibitisha sababu halisi za vifo hivyo.
Serikali imesisitiza kuwa juhudi zimeimarishwa kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na:
• Kuongeza kasi ya uchunguzi wa kiafya kwa wagonjwa.
• Kuimarisha ufuatiliaji wa watu waliokutana na wagonjwa wanaoshukiwa.
• Kupeleka wataalamu wa afya na vifaa vya dharura mkoani Kagera.
Wananchi wanashauriwa kuchukua tahadhari zote za kiafya, ikiwemo kujiepusha na mawasiliano ya karibu na wagonjwa au maiti zinazohusishwa na dalili za Marburg. Pia, taarifa za mara kwa mara zitakuwa zikitolewa na mamlaka husika.

Comments