DCEA YATEKETEZA KILO 185 ZA ‘UNGA’


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini, kwa niaba ya Kamishna Jenerali, January 16, 2025 imeteketeza jumla ya kilo 185.35 za dawa za kulevya aina ya ‘unga’. Uteketezaji huo ulifanyika katika Dampo la Maji ya Chai lililopo wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha, na ni sehemu ya juhudi kubwa za kupambana na matumizi ya dawa za kulevya nchini.


Aidha, DCEA iliteketeza kilo 154.35 za mirungi na kilo 31 za bangi mbichi. Jumla ya watuhumiwa watano walikamatwa kwa makosa ya kupatikana na dawa hizo. Uteketezaji huu ulifanyika kwa kuzingatia taratibu za kisheria, na mahakama ya Wilaya ya Arumeru iliridhia uchomaji wa vielelezo hivyo kwa kuwa dawa hizo zinaweza kuwa hatari kwa afya ya binadamu endapo zitaendelea kuhifadhiwa.


Mkuu wa Oparesheni kutoka DCEA Kanda ya Kaskazini, Innocent Masangula, alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na mamlaka katika kupambana na dawa za kulevya. Aidha, Ofisa Sheria wa DCEA, Benson Mwaitenda, alisisitiza kuwa sheria dhidi ya dawa za kulevya ni kali, na anayejihusisha na biashara hiyo anaweza kufungwa hadi miaka 30 au kifungo cha maisha. Vifaa vilivyotumika kusafirisha dawa hizo au nyumba zilizotumika kama maghala yanaweza kutaifishwa na kuwa mali ya serikali baada ya uchunguzi.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA