DKT. SAMIA ATANGAZA KESI MOJA YA VIRUSI VYA MARBURG


Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametangaza kubainika kwa mgonjwa mmoja aliyeambukizwa virusi vya Marburg (MVD) katika Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera. Rais Samia alizungumza mjini Dodoma katika mkutano wa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambapo alithibitisha kuwa kisa hicho kimepata uthibitisho baada ya vipimo vya kitaalamu kufanywa katika Maabara ya Kabaile na kuthibitishwa jijini Dar es Salaam.


Wiki iliyopita, Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, alikanusha taarifa za kuwepo kwa ugonjwa wa Marburg nchini, akisema hakuna mtu aliyepatikana na maambukizi ya virusi hivyo. Hata hivyo, Rais Samia amesema hii sio mara ya kwanza kwa Tanzania kukumbwa na mripuko wa Marburg, kwani ugonjwa huo ulianza kuibuka kwa mara ya kwanza Machi 2023 katika mkoa wa Kagera.


Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kudhibiti maambukizi na kuhakikisha usalama wa wananchi, huku wananchi wakitakiwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA