SHULE HII AUSTRALIA HURUHUSU WANAFUNZI KUVUTA SIGARA SHULENI
Chuo cha Arethusa College, Queensland, Australia, kimezua mjadala kwa kuruhusu wanafunzi kuchukua mapumziko ya kuvuta sigara shuleni.
Taarifa zinaonyesha kuwa karibu wanafunzi 50 hutumia eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kuvuta sigara, hatua ambayo shule inadai husaidia kudhibiti uraibu wao na kuzuia athari mbaya kwa masomo yao.
Uongozi wa shule unasema hatua hiyo inalenga kuzuia tabia hatarishi kama kuruka shule au kuvuta sigara kwa siri. Ingawa wanadai kupata kibali cha wazazi, baadhi ya wazazi wameonyesha wasiwasi, wakidai kuwa hatua hiyo imesababisha watoto wao kuanza kuvuta sigara.
Arethusa College ni shule inayolenga wanafunzi waliotatizika katika mfumo wa kawaida wa elimu, lakini sera hii imeibua mjadala mkubwa kuhusu jukumu la shule katika malezi bora ya wanafunzi.

Comments