VIONGOZI WAPYA WA SYRIA WATANGAZA KRISMASI KUWA SIKUKUU YA TAIFA


Syria imechukua hatua ya kihistoria baada ya viongozi wapya wa serikali kutangaza rasmi kwamba Krismasi, tarehe 25 na 26 Desemba, itakuwa sikukuu ya taifa. Uamuzi huu wa Disemba 24,2024 unalenga kuheshimu na kutambua mchango wa jamii ya Wakristo nchini humo, huku taifa likijaribu kuonyesha mwelekeo wa ujumuishi baada ya kuangushwa kwa utawala wa Rais Bashar al-Assad.


Hata hivyo, hali ya wasiwasi bado ipo, hasa baada ya matukio ya uchomaji wa mti wa Krismasi katika mji wa Kikristo wa Al-Suqaylabiyah, hali iliyosababisha maandamano ya Wakristo wakitaka usalama zaidi kwa maeneo yao ya ibada na urithi wa kidini.


Licha ya ahadi za uongozi mpya, ambao unajumuisha wanachama wa kundi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS), jamii ya Wakristo inabaki na mashaka kutokana na historia ya kundi hilo. Wito wa kuhifadhi haki na usalama wa wachache unazidi kushika kasi wakati taifa hilo likianza safari mpya ya kisiasa.


Hatua hii inatafsiriwa kama ishara ya matumaini, lakini Wakristo wa Syria wanataka vitendo zaidi kuliko maneno ili kuhakikisha haki zao na urithi wao unalindwa.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA