FAUSTINE NDUNGULILE AMEFARIKI DUNIA


Mbunge wa Kigamboni DK Faustine Ndugulile amefariki dunia tarehe 27 Novemba 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.


Taarifa ya kifo hicho imetolewa na Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson. Amesema taarifa zaidi kuhusu msiba huo itatolewa.


Dk Ndugulile Alikuwa Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Dunia Kanda ya Afrika (WHO) ambaye alipaswa kuanza majukumu hayo mapya Februari 2024.


"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu allaze roho ya marehemu mahali pema peponi,"amesema Spika

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA