RAIS DKT. SAMIA AIHAMISHA SEKTA YA HABARI KUTOKA WIZARA YA MAWASILIANO KWENDA WIZARA YA UTAMADUNI NA MICHEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Disemba 8, 2024 ametangaza mabadiliko ya kiutendaji kwa kuihamisha Sekta ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Aidha Dkt. Samia sambamba na hilo amefanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt.Moses Kusiluka, uteuzi na mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:
MAWAZIRI WALIOTEULIWA
2. Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.):
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
3. Mhe. Jerry William Silaa (Mb.):
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
4. Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.):
Waziri wa Katiba na Sheria.
5. Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (Mb.):
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
6. Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb.):
Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
7. Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb.):
Waziri wa Ujenzi.
8. Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.):
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
WATEULE WENGINE
9. Bw. Gerson Msigwa:
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Msemaji Mkuu wa Serikali.
10. Dkt. James Henry Kilabuko:
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
11. Dkt. Stephen Justice Nindi:
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo anayeshughulikia masuala ya ushirika na umwagiliaji.
12. Dkt. Suleiman Hassan Serera:
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara (amehamishwa kutoka Wizara ya Kilimo).
BALOZI WALIOTEULIWA
13. Bw. Anderson Gukwi Mutatembwa:
Balozi, atapangiwa kituo cha kazi.
14. Bw. Mobhare Matinyi:
Balozi, atapangiwa kituo cha kazi.
15. Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad:
Balozi, atapangiwa kituo cha kazi.
16. Kamishna wa Polisi CP. Suzan Kaganda:
Balozi, atapangiwa kituo cha kazi.
17. Bw. Thobias Makoba:
Balozi, atapangiwa kituo cha kazi (aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali).
WATEULE WA NYADHIFA NYINGINE
18. Prof. Mohamed Yakub Janabi:
Mshauri wa Rais Masuala ya Afya na Tiba. Ataendelea pia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
UAPISHO
Uapisho wa viongozi walioteuliwa utafanyika Ikulu Ndogo, Tunguu Zanzibar tarehe 10 Desemba, 2024 kuanzia saa 5:00 asubuhi.
Aidha, Mabadiliko haya yanalenga kuimarisha utendaji wa Serikali katika kuhudumia wananchi na kusimamia maendeleo ya taifa.

Comments