KANISA KUU LA NOTRE DAME LAFUNGULIWA RASMI HUKO PARIS, UFARANSA

Kanisa Kuu la kihistoria la Notre Dame limefunguliwa rasmi Desemba 7, 2024 jijini Paris, Ufaransa, baada ya miaka mitano ya ukarabati kufuatia moto mkubwa ulioteketeza sehemu kubwa ya jengo hilo mwaka 2019. 


Hafla ya ufunguzi huo imehudhuriwa na viongozi wa kimataifa, wakiwemo Rais wa Mteule wa Marekani Donald Trump, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, pamoja na wageni mashuhuri kutoka sehemu mbalimbali duniani.


Ufunguzi huu umekuwa tukio muhimu linalodhihirisha urejeshaji wa urithi wa kihistoria wa Ufaransa. 


Kazi ya ukarabati wa kanisa hilo ilihusisha maelfu ya mafundi stadi, wasanifu, na wahandisi, ambao walihakikisha jengo hilo linarejeshwa kwa mwonekano wake wa awali bila kupoteza thamani yake ya kihistoria.


Kanisa hilo, ambalo ni mojawapo ya alama kuu za utamaduni wa Ufaransa na kivutio cha mamilioni ya watalii kila mwaka, sasa limefunguliwa kwa ajili ya waumini na wageni wanaotaka kulishuhudia baada ya kazi kubwa ya ukarabati kukamilika.


 

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA