SHUGHULI ZA UOKOZI KARIAKOO KUHITIMISHWA LEO


 Ni siku ya 10 sasa tangu maafa yatokee ya kuporomoka kwa jengo katika soko la biashara la kimataifa kariakoo asubuhi ya jumamosi tarehe 16 Novemba 2024 na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.


Serikali imekuwa ikishughulikia maafa hayo kwa kuokoa watu, kutibu  majeruhi na kuzika waliopoteza maisha katika  maafa hayo ambapo kufikia  leo Jumanne, Novemba 26, 2024, Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika eneo la jengo lilipoporomoka amesema amesema shughuli ya uokozi imefikia tamati leo Jumanne Novemba 26.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA