WATU 14 WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 8 WAJERUHIWA KWA AJALI
Watu 14 wamefariki dunia na wengine 8 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori la mizigo lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Morogoro na coaster iliyokuwa inatokea Morogoro kwenda Dar usiku wa kuamkia leo, eneo la Mikese, barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Nkungu Daniel, amethibitisha kupokea miili ya marehemu na majeruhi, na kusema kwamba miili ya waliokufa bado haijatambuliwa. Alisema kuwa kati ya waliokufa, wanaume ni 8 na wanawake ni 6, huku majeruhi wakipatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, alitembelea hospitali hiyo alikozuiliwa majeruhi, na aliwataka wananchi kufika hospitalini hapo ili kutambua miili ya ndugu zao waliopoteza maisha. Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa jamii katika kutambua miili na kusaidia familia za waathirika.
Ajali hiyo ilihusisha madereva wawili, ambao kwa bahati mbaya walipoteza maisha.

Comments