POLISI MSUMBIJI WAKABILIANA NA WAANDAMANAJI BAADA YA UCHAGUZI WENYE UTATA
Polisi wa Msumbiji jana wamelazimika kurusha mabomu ya moshi (machozi) na risasi kwa waandamanaji katika mji mkuu Maputo waliokuwa wamekusanyika katika eneo la tukio ambapo viongozi wawili wa vyama vya upinzani waliuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumamosi baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata.
Katika maandamano hayo polisi wameonekana wakiwatawanya umati. Adriano Nuvunga, Mkurugenzi wa Kituo cha Demokrasia na Haki za Kibinadamu cha Msumbiji, amesema kuwa waandishi wa habari wawili na mlinzi mmoja walipigwa na risasi lakini hawakujeruhiwa vibaya.
Msemaji wa polisi hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia hilo. Matokeo kamili ya uchaguzi wa kitaifa wa Oktoba 9 yanatarajiwa kutangazwa wiki hii, huku matokeo ya mapema yakionyesha kuwa chama tawala cha Frelimo kinatazamiwa kupata ushindi mwingine.
Frelimo imetawala nchi hiyo ya kusini mwa Afrika tangu mwaka 1975.
Mgombea huru wa urais Venancio Mondlane alisema kuwa mgomo wa kitaifa wa Jumatatu ulizingatiwa vyema na kuwaambia waandamanaji warudi nyumbani baada ya makabiliano na polisi. Biashara nyingi zilifungwa katika mitaa ya Maputo katikati mwa jiji zilikuwa kimya.

Comments