Kuagwa kwa Mwili wa Dk. Mwele Malecela leo





1. Mamia ya waombolezaji katika Jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Kassim Majaliwa wameongoza ibada ya kuaga mwili wa Dk.Mwele Malecela.


Dk.Mwele ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela ameagwa jana Februari 19, 2022 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa jijini Dodoma kwa ajili ya kuupumzisha mwili wake katika nyumba yake ya milele. Dk Mwele (58) aliyekuwa Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyopewa vipaumbele Shirika la Afya Duniani(WHO) alifariki dunia Februari 10 mwaka huu Mjini Geneva ,Uswiz alipokuwa akipatiwa matibabu.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA