BINTI ANAYEDAIWA KUWA WA PUTIN ABADILI JINA LAKE AKIWA PARIS


Binti anayedaiwa kuwa mtoto wa Rais Vladimir Putin, aliyezaliwa kutokana na uhusiano wake na msafishaji wa zamani Svetlana Krivonogikh, amekuwa akiishi Paris kwa jina tofauti na anafanya kazi kama DJ. 


Binti huyo, Luiza Rozova (au Elizaveta Olegovna Rudnova), mwenye umri wa miaka 21, alifuatiliwa na vyombo vya habari vya Ukraine kupitia rekodi za ndege zilizovuja. 


Inadaiwa kwamba Rozova ameacha jina lake la patronymic “Vladimirovna” na kutumia jina la “Olegovna”, ikiwa ni kiashiria cha uhusiano wake na rafiki wa karibu wa Putin aliyeaga dunia, Oleg Rudnov.


Rozova alizaliwa Machi 3, 2003, na jina la babake halikuorodheshwa kwenye cheti chake cha kuzaliwa. 


Anadaiwa kuwa mtoto wa uhusiano wa siri kati ya Putin na Krivonogikh, msafishaji wa zamani ambaye sasa ni miongoni mwa wanawake matajiri zaidi nchini Urusi. 


Krivonogikh ni mjumbe wa bodi ya Bank Rossiya, inayotumiwa na wasomi wa Urusi kuhamisha pesa. 


Kulingana na uchunguzi wa 2020 wa kundi la uchunguzi la Urusi Proekt, Putin na Krivonogikh waliingia katika uhusiano miaka ya 1990 kabla ya kuwa Rais na wakati bado alikuwa ameolewa na Lyudmila Shkrebneva. 


Mnamo 2003, alijifungua msichana, bila jina la baba kuorodheshwa katika rekodi rasmi.


Krivonogikh ana mali nyingi, ikiwa ni pamoja na nyumba huko Monaco na boti, na anamiliki hisa katika hoteli ya Igora Ski Resort nchini Finland.


Baada ya mzozo wa Ukraine kuzuka mwaka 2022, Rozova anayedaiwa kuwa mtoto wa Putin alifuta akaunti zake za mitandao ya kijamii kutokana na shutuma alizozipata kwa kuonyesha maisha yake ya kifahari. 


Pia alikanusha kufanana na Putin na kusema kuwa alikuwa akiishi kwa faragha na kutokujali habari za kisiasa.


Putin ametambulisha hadharani mabinti wawili Maria na Katerina kutoka kwa ndoa yake ya kwanza, lakini kumekuwa na uvumi kuhusu watoto wake wa siri, wakiwemo wawili na mwanadensi Alina Kabaeva, ingawa amekanusha hilo.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA