DKT. SAMIA AMTEUA DKT. MPOKI KUWA BOSI MPYA MOI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali leo nchini.
Aidha, amemteua Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).
Pia amemteua Bi. Joyce Gideon Mapunjo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Bi. Mapunjo anachukua nafasi ya Mhandisi Musa Iyombe ambaye amemaliza muda wake.
Taarifa za uteuzi huo zimetolewa leo 02 Disemba 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga.

Comments