BUNGE LAPITISHA MAREKEBISHO YA SHERIA 12 KUBORESHA UTEKELEZAJI
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Miswada Miwili ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya 2024 Januari 29, 2025, katika kikao cha pili cha Mkutano wa 18 wa Bunge hilo.
Miswada hiyo ni:
1. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mbalimbali (Na.3) wa Mwaka 2024 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments No. 3) Bill 2024)
2. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2024 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments No. 4) Bill 2024)
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari, amesema Miswada hiyo inalenga kufanya marekebisho kwenye jumla ya sheria 12 ili kuboresha utekelezaji wake na kuzifanya ziendane na mahitaji ya sasa kwa manufaa ya wananchi.
Miongoni mwa sheria zilizofanyiwa marekebisho ni Sheria ya Mawakili, Sheria ya Madini, Sheria ya Utumishi wa Umma, Sheria ya Kudhibiti Utakatishaji wa Fedha Haramu, Sheria ya Vyama vya Ushirika, na Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Joseph Mhagama, amesema marekebisho haya yataleta maboresho katika utekelezaji wa sheria, hivyo kusaidia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania.
Hizi ndizo sheria 12 zilizofanyiwa marekebisho kupitia Miswada Miwili ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya 2024:
1. Sheria ya Mawakili – Sura ya 341
2. Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu – Sura ya 3
3. Sheria ya Huduma za Jamii – Sura ya 291
4. Sheria ya Shirika la Soko la Kariakoo – Sura ya 132
5. Sheria ya Madini – Sura ya 123
6. Sheria ya Utumishi wa Umma – Sura ya 298
7. Sheria ya Kudhibiti Utakatishaji wa Fedha Haramu – Sura ya 423
8. Sheria ya Vyama vya Ushirika – Sura ya 211
9. Sheria ya Tasnia ya Pamba – Sura ya 201
10. Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji wa Kiuchumi – Sura ya 386
11. Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji – Sura ya 435
12. Sheria ya Ukaguzi wa Umma – Sura ya 418
Marekebisho haya yanalenga kuboresha utekelezaji wa sheria hizo ili ziendane na wakati na kuleta tija kwa wananchi.

Comments