MCHENGERWA: MIRADI YOTE NGAZI YA MSINGI ITANGAZWE KUPITIA NeST


 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na wakuu wa vitengo vya manunuzi kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa katika ngazi ya msingi inatangazwa kupitia mfumo wa NeST.


Akizungumza leo jijini Dodoma katika kikao kazi na wabunge, wakurugenzi wa halmashauri, makatibu tawala wasaidizi miundombinu na wakuu wa vitengo vya manunuzi, Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa utekelezaji wa miradi lazima ufuate sheria za manunuzi na kuanzia sasa utatangazwa kupitia NeST pekee.


Ameeleza kuwa baada ya mafunzo haya, wahusika wanapaswa kubadilika na kusimamia miradi kwa weledi na uaminifu ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana. Pia, ameitaka PPRA kuwajengea uwezo watumiaji wa NeST katika ngazi za msingi ili kupunguza changamoto wakati wa mchakato wa zabuni.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA