WATANZANIA WALIOKWAMA VITANI DRC WAOKOLEWA
Mapigano yaendelea kushika kasi, waasi wa M23 waendelea kusonga mbele
Raia wa Tanzania waliokuwa wamekwama katika machafuko yanayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hatimaye wameokolewa baada ya kuomba msaada kufuatia mapigano makali.
Watanzania hao walijikuta katikati ya vita baada ya waasi wa M23 kushambulia na kuteka maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na Goma. Wengi walilazimika kujificha katika eneo la Jambo Safari na Uwanja wa Ndege wa Goma, huku milio ya risasi na makombora ikiendelea kusikika karibu nao.
Mashirika ya misaada na vikosi vya usalama vya Kongo vilihusika katika juhudi za kuwaokoa raia hao, ambao walikuwa hatarini kutokana na hali mbaya ya usalama.
Mapigano kati ya waasi wa M23 na majeshi ya Kongo (FARDC) yanaendelea kushuhudiwa mashariki mwa DRC, huku hali ikiendelea kuwa mbaya zaidi, ikiwalazimu maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao.

Comments