MARAIS WA AFRIKA WAAZIMIA KUWAUNGANISHA WAAFRIKA MILIONI 300 KWENYE NISHATI
Trilioni 110/- zatengwa kwa ajili ya mpango wa MISSION300
Marais wa Afrika wameazimia kuchukua hatua kubwa katika kuhakikisha upatikanaji wa nishati barani Afrika, wakitenga jumla ya trilioni 110/- ili kuwaunganisha Waafrika milioni 300 kwenye huduma za nishati.
Mpango huo, unaojulikana kama MISSION300, unalenga kuboresha maisha ya mamilioni ya watu ambao bado hawajafikiwa na nishati ya uhakika, huku viongozi wakisisitiza umuhimu wa usimamizi bora wa fedha hizi ili kuhakikisha matokeo chanya kwa wananchi.
“Tunataka kuona matokeo chanya kwa hawa watu milioni 300 watakaoguswa na MISSION300, lakini tunasisitiza umuhimu wa kusimamia fedha vizuri,” alisema mmoja wa viongozi katika mkutano huo.
Mpango huu unatarajiwa kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya nishati, kupunguza umaskini wa nishati, na kuongeza fursa za kiuchumi kwa jamii mbalimbali barani Afrika.

Comments