RAIS DKT. SAMIA KUSHIRIKI MKUTANO WA DHARURA WA SADC NCHINI ZIMBABWE KUJADILI HALI YA ULINZINA USALAMA DRC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kusafiri leo Januari 31, 2025, kuelekea Harare, Zimbabwe kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Akiwa nchini Zimbabwe, Rais Dkt. Samia atashiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC ulioitishwa kujadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mkutano huo utaongozwa na Rais wa Zimbabwe na Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Dkt. Emmerson Dambudzo Mnangagwa.

Mkutano huu unafanyika kufuatia Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ Troika) pamoja na nchi zinazochangia askari katika Misheni ya SADC nchini DRC (SAMIDRC), uliofanyika Januari 28, 2025, chini ya uenyekiti wa Rais Dkt. Samia.NA USALAMA DRC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kusafiri leo Januari 31, 2025, kuelekea Harare, Zimbabwe kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Akiwa nchini Zimbabwe, Rais Dkt. Samia atashiriki Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC ulioitishwa kujadili hali ya ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mkutano huo utaongozwa na Rais wa Zimbabwe na Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Dkt. Emmerson Dambudzo Mnangagwa.

Mkutano huu unafanyika kufuatia Mkutano wa Dharura wa Utatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Organ Troika) pamoja na nchi zinazochangia askari katika Misheni ya SADC nchini DRC (SAMIDRC), uliofanyika Januari 28, 2025, chini ya uenyekiti wa Rais Dkt. Samia.

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA