TANZANIA KUBADILI NOTI ZA FEDHA NA ALAMA ZAKE

Benki Kuu ya Tanzania imeeleza kuwa serikali imeamua kuondoa kwenye mzunguko baadhi ya noti za zamani za shilingi ya Tanzania zilizotolewa kati ya mwaka 1985 hadi 2003 na noti ya shilingi mia tano iliyotolewa mwaka 2010. 

Tangu ilipoanzishwa mwaka 1966, Benki Kuu ya Tanzania imetoa matoleo mbalimbali ya noti na sarafu.Kwa historia ya matoleo ya Noti na sarfu zilizotolewa na Benki kuu ya Tanzania.

Noti hizi ni zile zenye alama maalum ya kutambua thamani ya shilingi ishirini, mia mbili, mia tano, elfu moja, elfu mbili, elfu tano, na elfu kumi.

Kuanzia tarehe 6 Januari 2025 hadi 5 Aprili 2025, wananchi wataweza kuweka au kubadilisha noti hizo kupitia benki na taasisi za kifedha, lakini mchakato huu utafanyika tu katika ofisi kuu na matawi ya benki na taasisi za kifedha, na hautafanyika kupitia mawakala.

Benki Kuu imetangaza kuwa itawapa mafunzo wafanyakazi wa benki na taasisi za kifedha ili kuhakikisha noti feki hazihusishwi katika zoezi hili. 

Wataelekezwa kuzingatia miongozo ya usalama, kupakia na kutambua noti bandia iliyoandaliwa na Benki Kuu mwaka 2015.

Benki Kuu pia imeeleza kwamba inatoa ruhusa kwa mabenki na taasisi za kifedha kupokea vipande vya noti ambavyo haviwezi kufikia bundi kamili kwa ajili ya kubadilishwa kwa thamani halisi.



 

Comments