VIONGOZI WA JUMUIA YA MADOLA WAKUTANA PACIFIC




VIONGOZI WA JUMUIA YA MADOLA  WAKUTANA PACIFIC


Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Jumuiya ya Madola (Common Wealth) wa 2024 umefunguliwa rasmi leo Ijumaa, Oktoba 25, katika visiwa vya Pacific huko Samoa.


Aidha, Viongozi wa Jumuiya hiyo watakutana  tena juma lijalo kuendelea na Mkutano huo.


Kwa kipindi hiki ni zamu ya Afrika kupata nafasi ya Katibu Mkuu baada ya miaka 20 kupita, huku kukiwa na utata kuhusu iwapo malipo ya fidia yanapaswa kujumuishwa kwenye ajenda za mkutano huo au la.


Wagombea watatu wanawania nafasi hiyo ya juu ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Shirley Ayorkor Botchwey; Waziri wa zamani wa biashara na viwanda wa Lesotho Joshua Phoho Setipa; na Waziri wa Mambo ya Nje wa Gambia Mamadou Tangara .


Rwanda inatoa wito kwa chama hicho chenye wanachama 56 kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kuondokana na "vikwazo na upendeleo" unaoendelea kuwarudisha nyuma wanawake na wasichana.

Je nini kitajiri? endelea kufuatilia katika blog hii.

Comments