JIFUNZE KUSAMEHE



*_JE WAJUA?_*


Kama ulikua huijui ndege ya LIBYA iliokuwa iende UGANDA kumsaidia Iddi Amini kwenye Vita vya KAGERA lakini ikapotezwa njia na kutua TANZANIA wacha nikufahamishe""


     Ilikuwa mwaka 1978-1979 majasusi wa Tanzania wakiongozwa na wataalamu wa mbinu, Meja Jeneral Kiwelu akiongoza Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini (MI) na Hassy Kitine akiongoza Tawi Maalumu la Ujasusi Tanzania (leo TISS), waliziongoza medani za vita nchini Uganda. 

   Wakati vita imepamba moto, Iddi Amini Dada wa Uganda aliomba msaada wa kijeshi kutoka Libya ambapo Rais Muammar Gadaffi alimsaidia askari, vifaru na makombora ya kisasa. 

   Taarifu za msaada wa kijeshi wa Libya ziliifikia Idara ya Ujasusi wa Kijeshi nchini Tanzania, iliyokuwa chini ya Meja Jenerali Kiwelu, wakati huo.

   Hakukuwa na chaguo zaidi ya kukabiliana na hali hiyo.

    Majasusi wa Tanzania, kwa kutumia wale waliopandikizwa kwenye uwanda wa mawasiliano eneo la maziwa makuu,

    Waliamua kuanza kuiteka (kuingilia mawasiliano) ya ndege hiyo ikiwa katika anga la Ethiopia. 

     Ndege hivyo ilipokaribia anga la Kenya, ilikuwa tayari inaongozwa kutoka kikosi cha ujasusi wa Kijeshi Ukonga jijini Dar es Salaam na kile cha   viunga vya Ngerengere Morogoro (Military Intelligence)  na ikaelekezwa kushuka uwanja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro badala ya kwenda Intebe, Uganda.

   Wakati rubani akikaribia kutua, Bendera za Uganda zilikuwa zikipepea uwanjani hapo kuashiria sasa yupo uwanja wa ndege wa Entebe, 

   Na alipotua tu kufumba na kufumbua Bendera za Tanzania zikaanza kupepea huku ndege hiyo ikiwa imezingirwa na kikosi maalumu cha JWTZ cha makomandoo kiitwacho Black Mamba. 

   Tukio hili ukifika Langley Makao Makuu ya CIA linatumiwa kama kama somo la mfano ambalo dunia ya ujasusi haijawahi kukumbana nalo.

   Laiti Kama Wanajeshi wa LIBYA wangefika salama Uganda na kuungana na Iddi Amini kupigana na Tanzania vita ingekua ngumu Sana kwa upande wa Tanzania,

    Vikosi vya siri kama hiki cha Tanzania vipo kila nchi duniani na kimsingi utendaji wake hauhusiani na "katiba za nchi wala haki za kibinadamu" kama ilivyo jeshi la kawaida

   Ndani ya vikosi hivi vya siri, ndimo kuna wadunguaji na kila aina ya miujiza, yote kwa yote ni kwa maslahi ya nchi husika. 

  Napenda niweke wazi kwamba, historia haisomwi ili kufufua chuki bali husomwa kujua yaliyopita, kuyasanifu yaliyopo na kupanga mipango kwa yajayo. 

   Hivi ndivyo tunavyosoma historia, iwe yenye kuhuzunisha, kufundisha ama kufurahisha,

   Tanzania ilipigana vita na Uganda, vita iliyoitwa Vita vya Kagera (ingawaje ilipiganwa hata ndani ya Uganda na Idi Amini Dada kufurushwa na kuikimbia Uganda).

   Vita vinahitaji rasilimali watu (askari na wataalamu wa kijeshi), fedha za kuendeshea vita na zana (za kivita na za mawasiliano ya kivita).

    Kwa mujibu wa taarifu rasmi na zinazothibitishwa na taarifu rasmi za kihistoria, Muammar Gaddafi alimpa Idi Amin Dada usaidizi kabambe ufuatao,

   Wanajeshi (Wapiganaji) elfu tatu (3,000) kutoka Libya na nchi zilizokuwa na mahusiano na Libya ambazo Gaddafi alizisaidia na zenye uzoevu wa mazingira ya vita; Vifaru aina ya T-54, T-55, BTR, APCs, BM-21, Katyusha MRLs;. MIZINGA; na Ndege za Kijeshi aina ya MiG-21s na Tu-22 Bomber.

   Wanajeshi wa Libya waliotumwa Uganda walikuwa katika makundi yafuatayo: Askari wa kawaida, Wanamgambo, makomandoo wa vita vya msituni (Wenye uzoevu wa vita vya kienyeji kutoka Jagwa la Sahara, maarufu kama Watuareg, waliopigana sana maeneo ya Tchad, Niger, Algeria na Darful). 

   Sasa walikuwa wamefika katika vita vya msituni wakikabiliana na majemadari wa vita kama Msuguli, Kiwelu, Mwita Kyaro .

    Baada ya kuwekwa Chini ya ulinzi walifungwa vitambaa usoni na kutawanyika kwenye kambi mbalimbali Nchini,

    Taarifa zikafika kwa Gaddafi kuwa ndege imetekwa baada ya kutua kimakosa Tanzania,

    Gaddafi akampigia simu Mwalimu Nyerere na kumuomba asiwauwe Askari wake yuko tayari kulipa pesa yoyote atakayo Lakini asiwauwe Askari wake,

   Nyerere hakuwa tayari kulipwa chochote alichofanya Mwalimu Nyerere ni kuwanyang'a vifaa vyote vikiwemo;- mabomu, bunduki na vyengine,

    Mwishowe Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere aliwasamehe na kuwaruhusu kurudi kwao Libya kwa ndege yao,

   Kitendo hicho kilimfanya Gaddafi amshukuru Sana Mwalimu Nyerere kwani kisheria za kijeshi walipaswa kuuliwa,

   Na Ghadafi akaomba aje Tanzania Mwalimu Nyerere akamruhusu na Urafiki kati ya Libya na Tanzania ukaimarika zaidi,

  Alivyokuja Mwalimu Nyerere akamuomba Ghadafi amjengee msikiti Butiama akamjengea,akamuomba pia amjengee Msikiti Dodoma akamjengea.

   Kama hiyo haitoshi Ghadafi alivyorudi kwake Libya alimtunuku Mwalimu Nyerere cheti Cha juu Cha heshima kinachotolewa na nchi hiyo kwa kitendo alichokifanya.

   Ndege yenyewe iliotekwa kutoka Libywa ni hiyo hapo.

   Jifunze kuwasamehe watu waliokukosea usiweke kinyongo moyoni na usilipe kisasi.

 

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA