MBIO ZA MWENGE DAR ES SALAAM

 


RAS RUGWA  APOKEA MWENGE WA UHURU KUTOKA  MKOA WA PWANI


*- Ataja ratiba ya Mwenge kukimbizwa Dar es Salaam*


*-Asisitiza Umuhimu wa Mwenge huu, Kauli Mbiu na Ujumbe wake*


*- Ataja thamani ya Miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru*


*-Akabidhi  Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni ambapo DC huyo akiri kuupokea na kuukimbiza katika Wilaya yake*


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam *Ndg. Hassan Rugwa* amepokea Mwenge wa Uhuru Leo tarehe 10 Aprili 2022 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Bunju "A" ukitokea Mkoa wa Pwani


Baada ya kuupokea Mwenge huo wa Uhuru *Ndg. Hassan Rugwa* ametaja ratiba ya ukimbizwaji wa  Mwenge katika Mkoa wa Dar es Salaam kuwa tarehe 10/05/2022 Utakimbizwa Kinondoni, tarehe 11/05/2022 Utakimbizwa Ubungo, tarehe 12/05/2022 Ilala, tarehe 13/05/2022 Kigamboni na kumalizika Temeke tarehe 14/05/2022 ambapo tarehe 15/05/2022 utakabidhiwa *Mkoa wa Kusini Pemba*


Aidha *Katibu Tawala* amesisitiza Umuhimu wa Mwenge  wa Uhuru wa 2022 unaosisitiza Sensa ya Watu na Makazi chini ya Kauli Mbiu *" Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo; Shiriki Kuhesabiwa tuyafikie Maendeleo ya Taifa"* na Ujumbe wa Kudumu wa Mbio za Mwenge kuhusu Mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya, Lishe na Rushwa


*Ndg. Hassan Rugwa* amesema jumla ya *Miradi 28* yenye thamani ya *Shilingi Bilioni 16. 4* itapitiwa na Mwenge wa Uhuru ambapo Miradi hiyo ipo iliyokamilika na iliyopo katika hatua mbalimbali za utekelezaji


Hata hivyo *Katibu Tawala* ameukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni *Mhe. Godwin Gondwe* ambaye amekiri kuupokea na kuukimbiza katika Wilaya yake ya Kinondoni


     *MWENGE OYEEEEEE*

Comments

Popular posts from this blog

RAIS SAMIA AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

SERIKALI YAHAKIKISHA USAFIRI BORA BRT AWAMU YA PILI

RAIS WA CABO VERDE ASISITIZA UTAWALA BORA NA ULIPAJI FIDIA KWA AFRIKA KATIKA UFUNGUZI WA MWAKA MPYA WA MAHAKAMA YA AFRIKA JIJINI ARUSHA