MBIO ZA MWENGE ZATUA KISARAWE
MWENGE WA UHURU WAFUNGUA MIRADI KISARAWE
WAZIRI DR JAFO AWAPONGEZA VIONGOZI KISARAWE
DC,DED WAPOKEA UFAFANUZI WA MWENGE KUYATEKELEZA KWA WAKATI ULIOPANGWA
NA.....,
PWANI-KISARAWE
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2022 Ndg SAHIL NYANZABARA GERARUMA amefungua miradi ya maendeleo mbalimbali kumi na mbili iliyopangwa katika wilaya ya kisarawe katika miundombinu ya barabara,afya,elimu, maji,vijana mikopo na uwezeshaji*
Mwenge wa uhuru umekuja kisarawe kumulika maendeleo ambayo viongozi wa serikali wanayasimamia kwa mujibu wa Sheria miradi ambayo wamepatiwa fedha za serikali kuja kwenu kwa ajili ya maendeleo ya jamii kwa ujumla,
*Serikali inawaletea maendeleo nyie wananchi katika sekta ya miradi ya Afya,Maji Elimu na miundombinu mbalimbali ili kupata urahisi wa maisha hivyo ni lazima wananchi kushiriki kuyajua haya ili kuwasimamia viongozi wetu na swala la kujua miradi katika Kijiji ni lako mwananchi alisisitiza Geraruma*
Hata hivyo nae mbunge wa Jimbo la kisarawe ambaye pia waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira Dr Selemani Said Jafo amesisitiza kwa viongozi wa mwenge wa uhuru kumulika kwa amani na upendo miradi yote iliyopendekezwa kwao pamoja na kutoa ujumbe wa mwenge kitaifa ambao wamekuja nao kisarawe,
*Niwaombe radhi kwa dharura niliyopata mdaa huu hapa hapa uwanjani Kuna sehemu natakiwa kufika ila ndugu zangu wa mbio za mwenge kitaifa naomba mwenge ukamulike kisarawe na kwengineko Tanzania bara na Zanzibar kwa amani na upendo maendeleo yote yaliyokusudiwa kwa wananchi wetu ili wayajue serikali inawahudumia kwa vitendo, vigezo, viwango vikubwa vya huduma alimalizia Dr Jafo,*
Aidha mwisho kabisa kiongozi wa mwenge wa uhuru aliendelea kwa kutoa maelekezo ya mwenge kwa mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji kwa mradi wa ujenzi wa zahanati ya Palaka ambao umeonekana kuwa na mapungufu ya kitalamu zaidi,
*Ndugu Mkuu wa wilaya kisarawe mwenge wa uhuru umefika hapa kufungua zahanati ya Kijiji hiki Cha Palaka ila mwenge umegundua mapungufu ya kitaalamu hivyo naagiza kwako DC na kamati yako hapa palaka usimamie kwa wakati haya maboresho ya mapungufu yaliyojitokeza ndani ya wakati ili wananchi waweze kupata huduma ya afya ya Serikali kwa wakati kwa mama, watoto na wazee na watanzania mbalimbali alimalizia GERARUMA*
*Jumla ya shughuli za mwenge mwaka huu wilaya kisarawe ni pamoja Kuzindua zoezi la anuani za makazi kiwilaya, kupokea taarifa ya mandalizi ya zoezi la sensa ya watu na maakazi ya mwaka 2022, Kuzindua club ya wapinga rushwa, Kuzindua Madarasa mawili ya P4r, na Madarasa matatu ya Uviko19,Kuzindua mradi wa maji mengwa, kutembelea kikundi Cha Vijana kujionea shughuli wanazozifanya kutokana na mikopo ya halmashauri,*
*kuweka jiwe la msingi jengo la OPD/RCH na nyumba ya mtumishi zahanati ya palaka, kupokea taarifa dhidi ya magonjwa ya mlipuko,dawa za kulevya, ukimwi, Kuzindua daraja Box culvert katika barabara ya kiluvya makurunge, kutembelea mradi wa maziwa wa CHAWAKIM, Kukabidhi chango wa mwenge wa uhuru kwa ajili ya ukarabati wa darasa shule ya msingi kiluvya B, Mwisho mwenge kisarawe mwaka 2022 umekimbia Kilometa 192.99.*
Ujumbe wa mwenge wa uhuru mwaka 2022 *SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO SHIRIKI KUHESABIWA TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA*

Comments