TIZAMA TFS WALICHOFANYA MSITUNI
TFS YASHIRIKI KIKAO CHA UWEKEZAJI KUTANGAZA UTALII WA MISITU.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishina wa Uhifadhi TFS Profesa Dos Santos Silayo tarehe 17/05/2022 jijini Dar es salaam Mhifadhi Mkuu Zainabu Bhungwa amesema kikao hicho kati ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Mh Juma Selemani Mkomi na Wawekezaji kutoka Ufaransa utaleta tija katika kuutangaza utalii wa Misitu.
Bi Zainabu amesema kupitia kikao hicho TFS imepata nafasi ya kuwaeleza wawekezaji hao fursa za uwekezaji kwenye Vivutio vya Utalii vinavyosimamiwa na TFS.
"Kikao hiki ni muhimu kwa TFS, tumeweza kuwaeleza Wawekezaji fursa za kuwekeza kwenye Vivutio vyetu, kama ilivyo kwa Mheshimiwa Rais kupitia filamu ya Tanzania The Royal tour anavyotangaza utalii, sisi TFS pia tunamuunga mkono kupitia Vivutio vyetu vya Utalii kwenye Hifadhi za Misitu." Bi Zainabu.
Awali katika kikao hicho Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Mh Juma Selemani Mkomi amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia kuwa Tanzania ni mahali sahihi kwa uwezekezaji wa Miundombinu na huduma za Utalii.
"Nawakaribisha sana Tanzania na niwahakikishie tu kwamba mkiwekeza Tanzania, mnaweza sehemu sahihi "Mhe Mkomi.
Taasisi nyingine zinazoshiriki kikao hicho ni TAWA na TANAPA.

Comments