MWANAMKE AMUUA MUMEWE KWA AJILI YA MALI
Mwanamke mmoja kutoka Telangana nchini India, anadaiwa kumuua mume wake kwa ajili ya Mali yenye thamani ya shilingi Milioni 8, na kusafiri umbali wa kilometa 800 Kutupa Mwili wake.
Mwanamke huyo anadaiwa kumuua mumewe katika eneo la Uppal la Telangana nchini India.
Taarifa ya leo kutoka jeshi la Polisi nchini humo imesema kuwa waliwakamata watu watatu mke wake Niharika, mpenzi wake Nikhil na mshtakiwa mwingine, Ankur, ambao walitekeleza njama ya mauaji kwa pesa za mfanyabiashara huyo na kuutupa mwili huo.
Inadaiwa mwanamke huyo alimuua mumewe, mfanyabiashara Ramesh mwenye umri wa miaka (55), huko Uppal baada ya kukataa kuhamisha mali ya thamani ya milioni 8 kwa jina lake.
Akiwa na washtakiwa wengine wawili, baadaye aliendesha gari na mwili hadi shamba la kahawa na kuuchoma moto.
Uchunguzi ulianza polisi walipopata mwili usiojulikana, uliochomwa katika shamba la kahawa uliokiwa vigumu kuutambua.
Wakati wa uchunguzi wa awali, polisi walichanganua picha za CCTV na kuona gari jekundu lililosaidia uchunguzi huo.
Gari hiyo iliyosajiliwa kwa jina la Rameshi (marehemu) ambaye mke wake aliandikisha malalamiko ya kupotea kwa gari hiyo.
Polisi waliwasiliana na wenzao wa Telangana kwa uchunguzi wa njama ya mauaji ya mfanyabiashara huyo.
Polisi katika mahojiano walibaini aliyehusika ni mke wake ambaye wakati wa kuhojiwa, alikiri kumuua mumewe na kutaja washirika wengine.
Katika mahojiano zaidi na polisi mwanamke huyo alifichua kwamba aliolewa na Ramesh, katika ndoa ya pili. Wakati huo huo, alikuwa kwenye uhusiano na mwanaume mwingine aitwaye na Nikhil aliyemshawishi kumuua mumewe Ramesh ili kupata utajiri wake.

Comments