WANAJESHI WA KOREA KASKAZINI KUJIUNGA NA JESHI LA URUSI HIVI KARIBUNI
WANAJESHI WA KOREA KASKAZINI KUJIUNGA NA JESHI LA URUSI HIVI KARIBUNI
Kikosi cha wanajeshi 3,000 wa Korea Kaskazini hivi karibuni kitaungana na wanajeshi wa Urusi katika kupigana na Ukraine, kuashiria kuingia kikamilifu kwa mji wa Pyongyang wa Korea Kaskazini katika vita.
Vyanzo vya kijasusi vilisema kitengo hicho kimekuwa kikifanya mazoezi kwa siri katika Mashariki ya Mbali ya Urusi kabla ya kutumwa kama sehemu ya kikosi cha anga cha Urusi. "Wanaitwa Kikosi cha Buryat," chanzo kikuu cha jeshi la Ukraine kiliiambia Politico.
Buryatia ni eneo la mbali la Urusi linalopakana na Mongolia ambalo Kremlin imelenga sana kuajiri wanajeshi.
Tafiti zinaonyesha kuwa Korea Kaskazini ina wanajeshi milioni moja wasio na uzoefu wa mapigano na historia ya vita. Jeshi lao halina mafunzo makali, Hii inaonyesha kuwa Urusi inaweza isiwe na nguvu kama inavyodhaniwa, kwani Putin sasa anategemea majeshi ya Korea Kaskazini.
Ni wazi kwamba Zelenskyy anafanya kazi bora katika kupunguza uvamizi wa Urusi.

Comments