AUSTRALIA ILIWAHI KUWA NA WATU MILIONI 25 KWA KANGAROO MILIONI 50
Idadi ya watu wa nchini Australia ilifikia milioni 25 mnamo Agosti 7, 2018 huku
kangaroo wakiwa wengi zaidi kuliko watu waliopo, Kangaroo wakiwa milioni 50 ikilinganishwa na watu takriban milioni 25.
Waaustralia walihimizwa kula nyama zaidi ya kangaroo kama njia ya kudhibiti idadi inayoongezeka.
Kufikia Machi 31, 2024, idadi ya watu nchini Australia ilikuwa watu milioni 27.1, ongezeko la 2.3% kutoka 2023 na Ukuaji huo ulichangiwa na uhamiaji wa ng'ambo, ambao ulichangia 83% ya ongezeko hilo, na ongezeko la asili, ambalo lilichangia 17% iliyobaki.
Makadirio ya Umoja wa Mataifa pia yanajumuishwa hadi mwaka wa 2100 yamekadiria idadi ya sasa ya Australia katika 2024 kuwa ni 26,699,482, huku idadi ya kangaroo ikiwa haijahuishwa.

Comments