Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ametaka wazazi na walezi wa watoto kutekeleza vyema majukumu yao katika malezi ili shule ziwe na watoto wenye nidhamu na maadili kwa kuwaandaa kuwa wataalamu na viongozi. Waziri Mhe. Dkt. Kijaji amesema hayo tarehe (09.01.2024) wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi ya miradi ya ujenzi ya madarasa na matundu ya vyoo katika shule za sekondari za Nyerere, Semkiwa, Makorola, na Foroforo zilizopo Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga. Amewakumbusha wazazi na walezi kufuata maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuchukua jukumu la kulea watoto kwa kusimama katika nafasi zao ili shule zinazojengwa zipate watoto wenye nidhamu na malezi bora. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji anafanya ziara ya kikazi ya siku tano Mkoani Tanga ambapo tayari amefanya ziara ya siku mbili katika Wilaya ya Lushoto na sasa yupo katika Wilaya ya Korogwe akimwakilisha Rais w...
Serikali ya Tanzania inatarajia kupokea mabasi 250 yanayotumia gesi asilia (CNG) kutoka China ndani ya miezi mitatu ijayo, hatua inayofungua njia kwa kuanza kwa huduma za Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya Pili jijini Dar es Salaam. Mabasi haya yameundwa kwa teknolojia rafiki kwa mazingira, yakilenga kupunguza gharama za mafuta, kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa, na kuimarisha ubora wa hewa katika jiji hilo. Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Tanzania kuelekea mfumo wa usafiri wa umma unaoendana na maendeleo endelevu. Awamu ya Pili ya mradi wa BRT, iliyokamilika kwa gharama ya dola milioni 160, ilianza ujenzi mwaka 2019 na sasa imekamilika. Njia hii inahusisha kilomita 20.3, ikianzia Gerezani na kupitia Kivukoni hadi Kawawa Kusini. Mradi huu umefadhiliwa kwa ushirikiano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa DART, kwa kushirikiana na mamlaka husika, amepewa jukumu la kuhakikisha mabasi haya yanaanza kutoa huduma mara tu y...
Comments